?>

Machafuko yanaendelea Darfur Sudan, mwito wa amani watolewa

Machafuko yanaendelea Darfur Sudan, mwito wa amani watolewa

Licha ya kutolewa miito ya kila namna ya kukomeshwa mapigano ya kikabila huko magharibi mwa Sudan, mapigano bado yanaendelea katika eneo hilo lenye historia ndefu ya machafuko na mapigano.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Taarifa zinasema kuwa, machafuko hayo yamezushwa na wakimbizi wanaopinga uamuzi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kutaka kumalizwa operesheni ya kikosi cha UNAMID katika jimbo la Darfur na kubakisha operesheni ndogo tu ya kisiasa.

Machafuko hayo yametokea mwishoni mwa wiki hii katika mji wa Geneida huko Darfur Kusini baina ya makabila ya Fallata na Masalit. Fujo hizo zimewalazimisha maafisa wa Khartoum ambao wanafanya juhudi za kumaliza uasi na mgogoro katika nchi hiyo iliyotumbukia kwenye mgogoro hasa baada ya maandamano makubwa ya wananchi yaliyoishia kupinduliwa Rais Omar al Bashir wa nchi hiyo.

Viongozi wa kieneo katika eneo la Darfur Kusini huko Sudan wamesema kuwa, wanajeshi kadhaa wametumwa katika eneo hilo ili kukabiliana na mapigano ya kikabila yaliyoshtadi huko magharibi mwa Sudan.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni