?>

Madai yasiyo na msingi ya Katibu Mkuu wa NATO dhidi ya Iran; kuushabikia utawala haramu wa Israel

Madai yasiyo na msingi ya Katibu Mkuu wa NATO dhidi ya Iran; kuushabikia utawala haramu wa Israel

Katibu Mkuu wa Muungano wa Kijeshi wa NATO ametoa madai yasiyo na msingi kuhusiana na uwezo wa kiulinzi na kisilaha wa Iran.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Jens Stoltenberg amesema mjini Brussels Ubelgiji katika mazungumzo yake na Yair Lapid, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa utawala haramu wa Israel kwamba, uwezo wa kiulinzi wa makombora na shughuli za nyuklia za Iran ambazo kimsingi ni za amani, eti zinatia wasiwasi. Katibu Mkuu wa NATO ametoa madai hayo yasiyo na mashiko katika hali ambayo, hajaashiria hata kwa mbali tishio la silaha za nyuklia za utawala ghasibu kwa Israel kwa usalama wa eneo la Asia Magharibi na ulimwengu kwa ujumla.

Jens Stoltenberg anatoa matamshi hayo ya uzushi kwamba, eti Iran ni tishio kwa usalama wa eneo katika hali ambayo, uvamizi wa Israel pamoja na hatua ya utawala huo ghasibu ya kutofungamana na Mkataba wa Kuzuia Uzalishaji na Usambazaji wa Silaha za Nyuklia (NPT) ndio daghadagha na wasiwasi mkuu wa eneo hili la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati).

Kinyume na matamshi ya Katibu Mkuu wa NATO, kwa mujibu wa ripoti za Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA), shughuli zote za miradi ya nyuklia ya Iran ni za amani na zinafanyika chini ya usimamizi na uangalizi wa wakala huo. Aidha kwa mujibu wa itikadi ya kidini na kufungamana kwake na mikataba ya kimataifa, hakuna wakati ambao Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilifikiria kuchukua hatua za kutaka kuwa na silaha za nyuklia; kwani kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu kufanya hivyo ni haramu.

Ukweli wa mambo ni kuwa, matamshi ya Jens Stoltenberg, Katibu Mkuu wa Shirika la Kijeshi la NATO ni kukariri tuhuma na madai yasiyo na msingi ya viongozi wa utawala dhalimu wa Israel pamoja na waungaji mkono wao dhidi ya Iran, ambao wanafanya njama za kutoa matamshi hayo ili kuficha siasa zao za kufarakanisha.  Katibu Mkuu wa NATO anatoa tuhuma hizo katika hali ambayo, kuna maswali mengi ambayo yamebakia bila majibu kuhusiana na nafasi ya shirika hilo na ufanyaji mambo kinyume na majukumu yake kuhusiana na maslahi ya nchi wanachama na kulinda amani na usalama wa eneo.

Muhammad-Reza Norouzpour, mweledi na mchambuzi wa masuala ya kisiasa anaashiria nukta hii kwamba, shirika la NATO kabla ya kuanza kutoa nasaha kwa wengine, linapaswa kuboresha heshima na itibari yake iliyoporomoka ikiwa ni matokeo ya kushiriki katika jinai za kivita huko nchini Afghanistan na maeneo mengine ya dunia.

Kama ilivyokuja katika taarifa ya ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Brussels, Ubelgiji ya kulaani matamshi yaliyo dhidi ya Iran ya Jens Stoltenberg, Katibu Mkuu wa muungano wa kijeshi wa NATO wakati alipokuwa akizungumza katika mkutano na Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa utawala haramu wa Israel ni kuwa, matamshi hayo ni ya upotoshaji na yasiyozingatia uhalisia wa mambo. Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umesema katika taarifa hiyo kwamba,  kusimama pamoja na mwakilishi wa utawala ambao siyo mwanachama wa mkataba wa NPT wa kuzuia usambazwaji silaha za nyuklia au mkataba wowote wa kimataifa wa kuweka chini silaha ni hatua isiyoweza kusaidia katika itibari ambayo Katibu Mkuu wa NATO anadai kuwa nayo.

Filihali baada ya kupita miaka 20 ya Marekani na NATO kuweko kwao kijeshi nchini Afghanistan, nchi hiyo ingali inataabika kwa vita, utumiaji mabavu, ukosefu wa amani na magendo ya mihadarati.

Hali ya Afghanistan na Iraq ni mfano mmoja tu wa utendaji mbovu wa shirika hilo la kijeshi. Kwa akali katika miongo miwili ya hivi karibuni sera za NATO katika eneo zimekuwa ndio chimbuko kuu la kuenea ukosefuu wa amani na vitendo vya utumiaji mabavu. Katika kikao chao mwaka 2010, wakuu wa Muungano wa Kijeshi wa NATO waliandaa malengo ya miaka 10 ya shirika hilo la kijeshi. Mhimili mkuu wa hati tajwa ulikuwa ni kutangaza tena NATO "usalama wa wote". Hata hivyo, NATO imefeli pakubwa katika kukabiliana na migogoro ya Syria na Iraq, kupambana na ugaidi, mgogoro wa wahajiri, ukosefu wa amani na uthabiti wa kisiasa na jinai za kuratibiwa za magenge ya kimataifa.

Ukweli wa mambo ni kuwa, lau kama Iran isinge ingia kwa wakati mwafaka katika medani ya kukabiliana na ugaidi wa Daesh nchini Syria na Iraq; bila shaka nchi wanachama wa NATO hii leo zingekuwa na hali nyingine kabisa. Kwa mtazamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuwa, njia pekee ya kukabiliana na vitisho vya kiusalama ni kutegemea uwezo wa ndani wa eneo. Huu ndio ule ukweli ambao unayatia kiwewe na kihoro madola ya magharibi na hata NATO yenyewe.342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*