?>

Maelfu ya wafungwa waachiliwa Mynamar huku hatima ya wengine ikiwa haijulikani

Mitambo mipya kabisa ya makombora ya vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezinduliwa katika gwaride maalum lililofanyika mapema leo kwa mnasaba wa "Siku ya Jeshi".


Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA:Maadhimisho ya Siku ya Jeshi yamefanyika mapema leo nchini kote, ambapo sambamba na gwaride maalum lililofanyika kwa mnasaba huo, mitambo mipya kabisa ya aina mbalimbali za makombora imezinduliwa pia.

Mitambo ya makombora iliyoundwa na wataalamu wa hapa nchini ya Sayyad 3 na 4, makombora ya Juhudi, kombora la kistratejia la S300 na S200 pamoja na mtambo wa kombora la Mirsad ilizinduliwa katika gwaride hilo lililofanyika leo.

Viongozi na wakuu wa jeshi na wa serikali walihudhuria hafla hiyo iliyofanyika kwa kuzingatia miiko na miongozo ya kiafya.

Kama ilivyokuwa katika mwaka uliopita wa 1399 Hijria Shamsia, gwaride la mwaka huu pia limefanyika katika vituo vyote vikuu vya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kote nchini kutokana na mazingira ya maambukizi ya virusi vya corona yanayotawala.

Tarehe 29 ya mwezi wa kwanza wa Farvardin, inayosadifiana na tarehe 18 Aprili inaadhimishwa hapa nchini Iran kuwa ni "Siku ya Jeshi".../

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*