?>

Majasusi wa Mossad waliokamatwa Iran walipanga kuua wanasayansi wa nyuklia

Majasusi wa Mossad waliokamatwa Iran walipanga kuua wanasayansi wa nyuklia

Afisa wa mahakama ya Iran amesema majasusi watatu wanaofanya kazi katika shirika la ujasusi la Israel Mossad, waliokamatwa mwezi Aprili, walikuwa wakipanga kuwaua wanasayansi wa nyuklia wa Iran.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Mehdi Shamsabadi, mwendesha mashtaka mkuu wa mkoa wa Sistan na Baluchistan ya Iran, aliwaambia waandishi wa habari Jumanne kwamba, "Kukamatwa kwa majasusi hawa wa Mossad kulifuatia operesheni ngumu ya kijasusi iliyochukua miezi minane."

"Ushahidi wa kutosha umekusanywa dhidi yao kwa njia ambayo hata hawakuonyesha pingamizi yoyote wakati hati ya kukamatwa kwao ilipotolewa," aliongeza.

Afisa huyo amebainisha kuwa baadhi ya wanachama wa kundi hilo la majasusi  walikamatwa katika maeneo ya kusini-mashariki ya nchi ya mkoa wa Sistan na Baluchistan huku majasusi wengine na watendaji wengine wakizuiliwa nje ya mkoa huo na vikosi vya usalama vya Iran. “Washtakiwa wamekiri kuwa baadhi yao walikuwa wakiwasiliana moja kwa moja na maafisa wa shirika la kijasusi la Mossad,” amesisitiza Shamsabadi.

Alisema kwa sasa kesi hiyo iko kwenye upelelezi wa awali na kwamba hati ya mashtaka itawasilishwa na kupelekwa mahakamani hivi karibuni. Afisa huyo hakutaja uraia wa majasusi waliokamatwa.

Katika taarifa tarehe 20 Aprili, Wizara ya Intelijensia ya Iran ilitangaza kukamatwa kwa majasusi watatu wa Mossad huko Sistan na Baluchistan.

Taarifia  hiyo ilisema wakati huo majasusi hao walihusika katika kusambaza taarifa za siri na nyaraka na kubainisha kuwa watatu hao walikamatwa kwa amri ya mahakama.

Hivi karibuni jopo moja la wanafikra Marekani lilisema kuwa stratijia ya Israel kuhusu Iran imekuwa ikifeli vibaya, na kuonya kwamba jibu kali la Tehran kwa chokochoko za utawala huo linaweza kuzua makabiliano ya kieneo.342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*