?>

Majenerali 50 wa jeshi la Ukraine wauawa katika shambulio la makombora

Majenerali 50 wa jeshi la Ukraine wauawa katika shambulio la makombora

Wizara ya Ulinzi wa Russia imesema majenerali zaidi ya 50 wa jeshi la Ukraine wameuawa katika shambulio la makombora ya Kalibr karibu na kijiji cha Shirokaya Dacha katika eneo la Dnepropetrovsk, katikati mwa Ukraine.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema idadi kubwa ya majenerali pamoja na maafisa wengine wa ngazi za juu wa Jeshi la Ulinzi la Ukraine walikuwa wamekusanyika katika kituo cha Kamandi Kuu kwa ajili ya kufanya mkutano wakati waliposhambuliwa kwa makombora hayo ya Cruise ya Russia.

Wizara hiyo imesema imetumia pia makombora ya Kalibr kulipiga ghala la silaha za Ukraine katika mji wa kusini wa Nikolayev. Miongoni mwa silaha za Ukraine ilizopokea kutoka kwa Wamagharibi na zilizoharibiwa kwenye shambulio hilo ni vifaru 10 aina ya M777 vya kufyatua makombora na magari 20 ya deraya. 

Jana Jumapili pia, Wizara ya Ulinzi ya Russia iliripoti kuwa, mashambulio mengine ya anga ya nchi hiyo yalisambaratisha maghala ya silaha za Ukraine katika maeneo ya Lysychansk na Kharkiv.

Miongoni mwa silaha za Ukraine zilizoteketezwa kwenye mashambulizi hayo ya ndege za Russia ni mabomu ya vishada na zana nyingine za kijeshi.


342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*