?>

Makamanda wa Israel: Stratijia ya Israel ya kukabiliana na Hizbullah, Hamas imefeli

Makamanda wa Israel: Stratijia ya Israel ya kukabiliana na Hizbullah, Hamas imefeli

Makamanda wawili wa ngazi za juu wa utawala wa Kizayuni wa Israel wanasema harakati za Hizbullah ya Lebanon na Hamas ya Palestina zinazidi kuimarika na kupata nguvu kiasi kwamba startijia za Israel za kukabiliana na harakati hizo mbili za Kiislamu zinafeli.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Brigedia Jenerali Zwika Vogel general wa kikosi askari wa akiba wa utawala haramu wa Israel amesema Hizbullah na Hamas mbali na kuwa zimeimarika kijeshi pia zina uwezo mkubwa wa vita vya kisaikolojia.

Katika mahojiano na Kanali ya 13 ya Televisehni ya Utawala wa Israel,  Voge amesema: " Hizbullah na Hamas zinazidi kuimarika huku sisi tukisema tuko katika mwaka wenye utulivu."

Ameendelea kusema kuwa: "Tumesahau kuwa hatuwezi kutembea kote Israel kama tukakavyo, usalama wa mtu binafsu umepungua. Tulipuuza Al Naqab na sasa hatuwezi kutemeblea tutakavyo maeneo ya kaskazini, ukweli huu unatuzaba vibao kila siku."

Kamanda huyo wa Israel amesema, Hamas ina maroketi zaidi ya 10,000 nayo Hizbullah ina zaidi ya 160,000. " Amesema kinachowakosesha wazayuni matumaini ni kuwa makombora hayo hayawezi kupata kutu na hivyo hatimaye yatavurumishwa kuelekea Israel.

Wakati huo huko kamanda mwingine wa kikosi cha akiba cha utawala wa Kizayuni wa Israel Kanali Kobi Marom amesema kuna matatizo katika siasa za ndani za Israel kutokana na Hamas. Katika mahojiano ya Televisehni kamanda huyo wa Kizayuni amekiri kuwa Hamas inapata ushindi dhidi ya Israel katika nyanja zote.

Hivi karibuni Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon alisema  Hizbullah itajibu papo hapo shambulio lolote la utawala huo haramu.

Aidha hivi karibuni Harakati za Hamas na Jihadul Islami za Palestina zimelaani vikali mwenendo wa baadhi ya watawala wa Kiarabu wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel na kusisitiza kwamba, muqawama na mapambano ya silaha ndio njia pekee ya kuzikomboa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*