?>

Makubaliano mapya ya Hamdok na al-Burhan yakabiliwa na upinzani Sudan

Makubaliano mapya ya Hamdok na al-Burhan yakabiliwa na upinzani Sudan

Makubaliano mapya yaliyofikiwa nchini Sudan baina ya Abdalla Hamdok na Jenerali Abdul-Fatah al-Burhan ambayo yanaonekana kama njia ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo baada ya mapinduzi ya kijeshi ya mwezi uliopita yamekabiliwa na upinzani mkali baada ya vyama kadhaa kuyapinga makubaliano hayo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Hatimaye kufuatia mashinikizo ya ndani na nje ya nchi, jeshi la Sudan jana lilikubali kumrejesha Abdallah Hamdok kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, sambamba na kuwaachia huru viongozi wa kiraia waliotiwa mbaroni baada ya kujiri mapinduzi ya kijeshi tarehe 25 Oktoba mwaka huu.

Hata hivyo kinyume ilivyotarajiwa, makubaliano hayo yamepingwa na baadhi ya vyama ukiwemo Muungano wa Wafanyakazi nchini Sudan ambao umesema katika taarifa yake kwamba, makubaliano ya wasaliti yaliyotiwa saini baina ya Abdalla Hamdok na Jenerali Abdul-Fatah al-Burhan hayakubaliki.

Taarifa ya muungano huo imeeleza kuwa, makubaliano hayo hayalengi na kuzingaia maslahi ya wananchi wa Sudan bali ni kwa maslahi ya waliotia saini makubaliano hayo.

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imeeleza kuwa, hayo ni "makubaliano ya kusalimu amri" ambayo kimsingi yanapingana na matakwa ya wananchi na kwamba, makubaliano hayo yanadhaminii malengo ya wafanya mapinduzi na ni khiyana na usaliti kwa damu za mashahidi ya mapinduzi ya Disemba.

Wakati huo huo, Chama cha Congresi ya Sudan nacho kimepinga makubaliano hayo ya Abdalla Hamdok na Jenerali Abdul-Fatah al-Burhan na kutaja makubaliano hayo kuwa ni ya pupa.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo ya kisiasa, Hamdok anatazamiwa kuunda baraza huru la mawaziri litakalojumuisha wasomi, huku jeshi likiafiki kuwaachia huru wafungwa wote wa kisiasa.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*