?>

Makundi yenye silaha yafanya mashambulizi kusini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Makundi yenye silaha yafanya mashambulizi kusini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Makundi yenye silaha jana Jumapili yalivamia na kufanya mashambulizi katika mji wa Bangassou wa kusini wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: limemnukuu Roosevelt Pierre-Louis, mkuu wa ofisi ya kieneo ya kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda Amani Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA) akithibitisha habari hiyo na kuongeza kuwa, mashambulizi hayo yaliyotokea katika mji wa Bangassou yameenea sehemu zote.

Baadhi ya duru za habari zinasema kuwa, waasi wameuteka mji huo wa Bangassou.

Jamhuri ya Afrika ya Kati imekumbwa na machafuko ya muda mrefu na mapigano yalishtadi baada ya kupinduliwa serikali ya Rais François Bozizé mwaka 2013. Mapigano makali yameripotiwa baina ya wanamgambo wa Seleka na wale wa Anti Balaka.

hadi hivi sasa ameshindwa kurejesha utulivu na amani nchini humo.

Wahanga wakuu wa machafuko wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ni raia wa kawaida hasa wanawake na watoto wadogo ambao wamelazimika kukimbia makazi yao.

Idadi ya wakimbizi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ni kubwa kiasi kwamba robo nzima ya jamii ya watu milioni 4 na laki 8 wa nchi hiyo, ni wakimbizi.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni