?>

Mamluki wa Imarati wanabaka wasichana wa Yemen Hudaydah

Mamluki wa Imarati wanabaka wasichana wa Yemen Hudaydah

Kitendo cha mamluki wa Umoja wa Falme za Kiarabu kuwabaka wasichana sita katika mkoa wa al-Hudaydah, magharibi mwa Yemen kimeibua ghadhabu na kulalamikiwa vikali katika pembe mbalimbali za nchi hiyo maskini ya Kiarabu.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Vyombo vya habari vya Yemen vimeripoti kuwa, jinai hizo za kutisha zilifanyika siku chache zilizopita katika maeneo ya  al-Juwayr na al-Suwaihra katika wilaya ya Hays mkoani Hudaydah.

Wakazi wa maeneo hayo ya mkoa wa bandari wa al-Hudaydah wametoa mwito wa kufukuzwa nchini humo mamluki hao wa Imarati haraka iwezekanavyo.

Shirika la Entesaf la Kupigania Haki za Wanawake na Watoto limelaani vikali ufuska huo na kubainisha kuwa, aina zote za udhalilishaji wa kingono zinapingwa vikali na sheria za kimataifa za ubinadamu, na kwamba mataifa yote yana wajibu wa kuwawajibisha kisheria wahusika.

Shirika hilo la kutetea haki za binadamu limeeleza bayana kuwa, Sura ya 27 ya Hati ya Nne ya Geneva iliyopasishwa Agosti mwaka 1949, inapiga marufuku ubakaji, kunajisi na aina zote za dhulma za kingono, na pia inasisitizia haja ya kulindwa raia nyakati za vita.

Shirika hilo limekosoa vikali kimya cha jamii ya kimataifa na hususan taasisi za Umoja wa Mataifa, mkabala wa jinai hizo na nyingine za kutisha wanazofanyiwa raia wa Yemen kila uchao.342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*