?>

Marais wa Misri na Afrika Kusini wajadili mzozo wa Bwawa la al-Nahdha

Marais wa Misri na Afrika Kusini wajadili mzozo wa Bwawa la al-Nahdha

Marais wa Misri na Afrika Kusini wamefanya mazungumzo kwa njia ya simu na kujadili hitilafu na mizozo iliyopo kuhusiana na kadhia ya Bwawa la al-Nahdha.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ambaye ni Mwenyekiti wa Kiduru wa Umoja wa Afrika amempigia simu mwenzake wa Misri Abdul-Fattah al-Sisi na kujadiliana naye kadhia ya Bwawa la al-Nahdha.

Ofisi ya Rais wa Misri imesisitiza kuwa, al-Sisi amesisitiza katika mazungumzo yake hayo na Ramaphosa msimamo wa Cairo wa kuheshimiwa makubaliano yaliyofikiwa huko nyuma baina yake na Sudan na Ethiopia kuhusiana na ujenzi wa Bwawa la al-Nahdha.

Jana Jumamosi pia, Rais Abdul-Fattah al-Sisi alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambaye nchi yake inatarajiwa kuchukua uwenyekiti wa kiduru wa Umoja wa Afrika majuuma machache yajayo ambapo mbali na kubadilishana mawazo kuhusiana na uhusiano wa Cairo na Kinshasa viongozi hao wamezungumzia mzozo wa Bwawa la al-Nahdha.

Bwawa la al Nahdha limejengwa katika umbali wa kilomita 15 kutoka kwenye mpaka wa Ethiopia na Sudan. Hadi mwezi Oktoba 2019, ujenzi wa bwawa hilo ulikuwa umeshamalizika kwa asilimia 70. Litakapoanza kufanya kazi bwawa hilo, litakuwa kituo kikuu zaidi cha kuzalisha umeme kwa kutumia maji, duniani.

Misri na Sudan zina wasiwasi kwamba ujenzi wa bwawa hilo utapunguza mgao wao wa maji na kusababisha tatizo kubwa la maji katika nchi hizo. Hadi sasa kumefanyika duru kadhaa za mazungumzo baina ya wawakilishi wa nchi hizo tatu lakini hayajakuwa na matokeo mazuri ya kuridhisha.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni