?>

Marekani; chanzo cha kusita kwa muda mrefu mazungumzo ya Vienna

Marekani; chanzo cha kusita kwa muda mrefu mazungumzo ya Vienna

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika mazungumzo ya simu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuwa, sera ghalati za mashinikizo ya kiwango cha juu za Marekani ndio sababu ya hali ya sasa ya mambo inayoshuhudiwa katika mazungumzo ya Vienna.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Hossein Amir-Abdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewasiliana kwa njia ya simu na Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kuashiria kuendelea kubadilishana ujumbe kati ya Iran na Marekani kupitia Umoja wa Ulaya na kukosoa azimo la karibuni la Seneti ya Marekani dhidi ya Iran. Abdollahian ameongeza kuwa: Upo ulazima kwa serikali ya Marekani kuchukua uamuzi wa kijasiri kwa mujibu wa  hali halisi ya mambo na hivyo kufidia makosa yake ya huko nyuma ili kufikia mapatano endelevu, imara na ya kiadilifu. 

Duru ya nane ya mazungumzo ya kuindolea Iran vikwazo ambayo ilianza tangu Disemba 27 mwaka jana, tarehe 11 mwezi Machi mwaka huu iliingia katika duru ya mapumziko kufuatia mapendekezo ya Josep Borrell Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya; na wawakilishi katika mazungumzo walirejea katika miji yao mikuu kwa ajili ya mashauriano ya kisiasa. 

Suala la kutoa hakikisho ili kuaminiwa, na kuwaondoa katika orodha yake nyekundu na katika safu ya vikwazo shakhsia wa kisheria lingali ni kati ya kadhia ambazo Marekani ikiwa upande uliokiuka mapatano ya JCPOA haijachukua maamuzi muhimu ya kisiasa kulipatia ufumbuzi suala hilo. 

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inasisitiza kuwa, kwa kuzingatia rekodi mbaya ya kutotekeleza ahadi nchi za Magharibi khususan Marekani katika kutekeleza kikamilifu makubaliano ya kimataifa ya JCPOA; pande husika katika mazungumzo zinapasa kufikia mapatano imara, ya kiadilifu na endelevu na hivyo kuandaa mazingira ya lazima ili Iran istafidi kikamilifu na manufaa ya kiuchumi ya JCPOA kupitia kupunguza wasiwasi wa madai ya nchi za Magharibi kuhusu miradi ya nyuklia ya nchi hii yenye malengo ya amani. 

Kwa msingi huo, timu ya mazungumzo ya Iran iliwasilisha mapendekezo na ubunifu wa kivitendo kwa pande nyingine katika mazungumzo ya Vienna; na hivyo mawasiliano na pande nyingine hufanyika katika fremu ya mistari myekundu. 

Katika hali ambayo mazungumzo ya Vienna yamekuwa yakisubiri Washington ichukue uamuzi wa kisiasa kuhusu masuala muhimu kadhaa yaliyosalia; seneti ya Marekani hivi karibuni imepasisha azimio la kudumisha vikwazo dhidi ya Benki Kuu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na pia mpango wa kuzuia kuondolewa vikwazo dhidi ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) iwapo serikali ya Joe Biden itarejea katika makubaliano ya JCPOA.  

Katika upande mwingine, Marekani inaendeleza wenzo wa  vikwazo na kustafidi na sera za undumakuwili na mashinikizo ya kiwango cha juu  dhidi ya Iran  katika hali ambayo kufikiwa makubaliano katika mazungumzo ya Vienna kunawezekana tu iwapo Washington itaachana na hatua zake za kupenda makuu na kuchukua hatua za wazi na kujenga hali ya kuaminiwa.  

Jarida la Politico linalochapishwa nchini Marekani limemnukuu kiongozi mmoja wa ikulu ya Marekani (White House) na kuandika: Msimamo wa Washingtoni ni huu kuwa haitaliondoa jina la SEPAH katika faharasa makundi ya yanayosemekana kuwa ni ya kigaidi madhali Iran haijachukua hatua mahsusi za kupunguza wasiwasi wa kiusalama uliopo mbali na  makubaliano ya JCPOA. Hii ni katika hali ambayo, msingi mkuu wa makubaliano ya JCPOA ni kuondolewa ipasavyo vikwazo vya kiuchumi mkabala wa Iran kutekeleza majukumu yake ya kinyuklia na wala hauhusiani na masuala ya kiulinzi na ya kisiasa ya Iran katika eneo. 

Hakuna shaka kuwa, kuendelea kustafidi Marekani na wenzo wa mashinikizo dhidi ya Iran, ukwamishwaji endelevu wa nchi hiyo katika mazungumzo ya Vienna na matakwa yake yaliyo nje ya makubaliano ya JCPOA, yote hayo yanaonyesha namna viongozi wa Washington  wanavyojielekeza katika mkondo wao huo wa siasa zilizogonga mwamba za serikali iliyotangulia ya nchi hiyo chini ya Donald Trump; na wala hawana azma thabiti ya kisiasa ya  kufidia makosa yao ya huko nyuma na kurejea katika JCPOA. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*