?>

Marekani yaiuzia silaha Misri licha ya serikali ya el Sisi kuendelea kukiuka haki za binadamu

Marekani yaiuzia silaha Misri licha ya serikali ya el Sisi kuendelea kukiuka haki za binadamu

Serikali ya Marekani imeidhinisha mauzo ya silaha zenye thamani ya dola milioni 200 kwa Misri licha ya serikali ya nchi hiyo kuendelea kuandamwa na shutuma za ukiukaji wa haki za binadamu.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Serikali ya Joe Biden, ambayo imeapa kukomesha uungaji mkono wake kwa mashambulio ya kijeshi ya Saudi Arabia dhidi ya Yemen na kuamua pia kuangalia upya mkataba wa mauzo makubwa ya silaha kwa Imarati, imesema imeidhinisha mkataba wa kuiuzia Misri makombora yenye thamani ya dola milioni 197.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeeleza katika taarifa kwamba, imeidhinisha mauzo hayo kutokana na mtazamo wa bunge la nchi hiyo kwamba Misri ingali ni mshirika muhimu wa kistratejia wa Washington katika Mashariki ya Kati.

Biden alikuwa amedai kwamba, atachukua msimamo mkali kuhusiana na Misri juu ya suala la haki za binadamu, hasa baada ya mtangulizi wake Donald Trump kuonyesha kuwa na ukuruba na rais wa nchi hiyo Abdel Fattah el Sisi aliyeripotiwa kumwita "dikteta wangu nimpendaye", -pamoja na mambo mengine-, kwa sababu ya ushirikiano wake na Israel.

Hayo yanajiri, mwanaharakati wa Kimarekani mwenye asili ya Misri Mohamed Soltan akiripoti kuwa, siku ya Jumapili, askari kanzu wa serikali ya Cairo walivamia nyumba za jamaa sita wa familia yake na kuwatia nguvuni wapwa wake wawili.

Soltan mwenyewe, ambaye ni mtoto wa mwanachama mwandamizi wa harakati ya Ikhwanul Muslimin, ambayo imepigwa marufuku na serikali ya Misri, alitiwa mbaroni Agosti 2013 baada ya Abdel Fattah el Sisi kuongoza mapinduzi ya kijeshi yaliyoiondoa madarakani serikali iliyochaguliwa kidemokrasia ya marehemu Muhammad Morsi.

Mohamed Soltan aliachiliwa huru mwaka 2015 na kuhamishiwa Marekani baada ya kuukana uraia wake wa Misri.../

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni