?>

Marekani yakataa ombi la Umoja wa Mataifa la kufutilia mbali vikwazo dhidi ya Ansarullah

Marekani yakataa ombi la Umoja wa Mataifa la kufutilia mbali vikwazo dhidi ya Ansarullah

Marekani imekataa ombi lililotolewa na Umoja wa Mataifa la kufutilia mbali uamuzi wake wa kuliweka jina la Ansarullah ya Yemen katika orodha ya makundi yanayotuhumiwa na Washington kuwa ni ya kigaidi.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Martin Griffiths, Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Yemen na wawakilishi wa nchi kadhaa katika kikao chao cha siku ya Alkhamisi usiku katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Washington walionya na kukosoa vikali hatua ya Marekani ya kuliweka jina la Ansarullah katika orodha yake ya  makundi ya kigaidi na kuitaka ifutilea mbali uamuzi wake huo, lakini Washington imekataa kulegeza msimamo kuhusu suala hilo.

Huku akilaani hatua hiyo ya Marekani, Griffiths amesema kuwa kuwekwa Ansarullah katika orodha hiyo kutavuruga juhudi zote ambazo zimefanywa hadi sasa kwa ajili ya kuleta amani na utulivu miongoni mwa pande zinazopigana nchini Yemen. Pia amesema kuwa uamuzi huo wa Marekani unapaswa kufutiliwa mbali kutokana na kuwa unakiuka haki za binadamu.

Akizungumza katika kikao hicho hicho cha siku ya Alkhamisi, Vasily Nebenzia, mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa alisema kuwa kutuhumiwa na Marekani Ansarullah kuwa ni kundi la kigaidi kutaharibu zaidi mgogoro wa kibinadamu unaoshuhudiwa huko Yemen.

Jumatatu iliyopita, Mike Pompeo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani alisema kuwa wizara yake tayari imeliarifisha kundi la Ansarullah kuwa miongoni mwa makundi ya kigaidi ya kigeni katika bunge la Congress, jambo ambalo limekabiliwa na upinzani mkali wa makundi, shakhsia, nchi na mashirika ya kimataifa.

Marekani imeachukua uamuzi wa kuituhumu Ansarullah kuwa ni kundi la kigaidi katika hali ambayo tokea mwaka 2015 Saudi Arabia, Imarati na nchi kadhaa za Kiarabu na kwa ushirikiano na msaada wa Marekani na Uingereza, zilianzisha hujuma kubwa ya kijeshi dhidi ya Yemen, ambayo ni nchi masikini zaidi katika ulimwengu wa Kiarabu.

Uvamizi huo wa kijeshi kufikia sasa umepelekea makumi ya maelfu ya Wayemen kupoteza maisha na kujeruhiwa na vile vile kulazimisha mamilioni ya wengine kuishi kama wakimbizi huku wakikabiliwa na matatizo chungu nzima ya njaa, magonjwa na uharibifu wa miundomsingi.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni