?>

Mashambulizi mapya ya Israel dhidi ya Wapalestina, matunda ya mwanzo ya "Muamala wa Karne"

Mashambulizi mapya ya Israel dhidi ya Wapalestina, matunda ya mwanzo ya

Ikiwa haujapita mwezi mmoja sasa tangu Rais Donald Trump wa Marekani alipozindua rasmi mpango uliopewa jina la "Muamala wa Karne", utawala wa Kizayuni wa Israel umeanzisha duru mpya ya vita na mashambulizi dhidi ya makundi na harakati za kupigania ukombozi za Palestina.

(ABNA24.com) Jeshi la Israel jana Jumapili lilishambulia kwa mizinga eneo la Ukanda wa Gaza na kumuua shahidi kijana wa Kipalestina, Mohammed Ali al-Naim aliyekuwa na umri wa miaka 27. Baada ya mauaji hayo askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel waliuvunjia heshima mwili wa kijana huyo kwa kutumia buldoza. Jinai hiyo ya Wazayuni imekabiliwa na hasira kali za wanaharakati wa Kipalestina.

Saraya al Quds, tawi la kijeshi la harakati ya Jihad Islami ya Palestina Jumapili ya jana ilivurumisha maroketi 20 dhidi ya vitongoji vya walowezi wa Kizayuni vilivyoko kandokando ya Ukanda wa Gaza.

Baada ya shambulizi hilo Israel ilishambulia eneo la Ukanda wa Gaza na kuua shahidi wapiganaji wawili wa Saraya al Quds.

Uchambuzi wa matukio hayo yote unaonesha kuwa, chanzo cha vita na mashambulizi haya mapya ya Israel ni tabia na sera za kutenda jinai za utawala huo habithi. Ukweli huu unaonekana wazi katika hatua ya askari wa utawala huo wa kuuvunjia heshima mwili na maiti ya kijana, Mohammed Ali al-Naim baada ya kumuua kinyama huko Gaza.

Mwenendo huu wa kutishia maisha ya Wapalestina na kuwavunjia heshima hata baada ya kuaua unaonesha waziwazi sera na siasa za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Wakati huo huo tunaweza kusema kuwa, duru mpya ya vita na mashambulizi ya Wazayuni dhidi ya raia wa Palestina ni matunda ya awali ya mpango wa kibaguzi wa Muamala wa Karne uliopendekezwa na Rais Donald Trump wa Marekani na kuzinduliwa katika ikulu ya Whote House tarehe 28 mwezi uliopita wa Januari.

Mpango huo unadhamini kikamilifu maslahi ya utawala haramu wa Israel na kukingia kifua jinai na uhalifu wa utawala huo dhidi ya Wapalestina.

Baada ya kuzinduliwa mpango huo, wachambuzi wa mambo walisema waziwazi kwamba hauwezi kutengeneza suluhu na mapatano na kwamba, kinyume chake, utazidisha uhasama na machafuko katika eneo la magharibi mwa Asia.

Duru mpya ya vita kati ya utawala wa Kizayuni wa Israel na harakati za mapambano za Palestina imeanza katika kipindi ambacho zimebakia siku 10 tu hadi siku ya uchaguzi wa Bunge la utawala wa Kizayuni ambao utakuwa wa tatu katika kipindi cha mwaka mmoja wa karibuni. Itakumbukwa kuwa, kabla ya uchaguzi wa tarehe 17 Septemba mwaka jana Benjamin Netanyahu alianzisha vita dhidi ya harakati za mapambano ya ukombozi huko Palestina na akafanya jitihada za kutumia suala hilo kwa malahi yake ya kisiasa.

Hata hivyo janja hiyo haikumuwezesha Netanyahu kushinda uchaguzi huo na zaidi ni kwamba, wakazi wa vitongoji vya walowezi vilivyoko kandokando ya Ukanda wa Gaza walikosoa sera zake za vita, na matokeo yake yalikuwa ushiriki mdogo sana wa wakazi wa maeneo hayo katika zoezi la uchaguzi.

Pamoja na hayo Netanyahu bado anacheza kamari ya vita na mashambulizi dhidi ya wakazi wa Gaza kama turufu ya kushinda uchaguzi ujao wa bunge.

Mwenendo huo wa kijahili ambao umezidisha chuki ya Wapalestina dhidi ya kile kilichopewa jina la Muamala wa Karne, unadhihirisha kwamba, Benjamin Netanyahu yuko katika siku za mwisho wa uhai wake wa kisiasa huko katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina.  

............
340 


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni