?>

Maulamaa wa Pakistan wakosoa filamu tata ya "Mwanamke wa Peponi"

Maulamaa wa Pakistan wakosoa filamu tata ya

Wanazuoni wa Kishia na maulamaa wengine wa Kiislamu nchini Pakistan wamelaani na kukosoa vikali filamu tata ya "Mwanamke wa Peponi" na kuitaja kuwa njama za maadui wa Uislamu wenye nia ya kupanda mbegu za chuki baina ya Waislamu.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Katika taarifa ya pamoja, wasomi hao wa kidini wa Pakistan wamesema filamu hiyo imetengenezwa kwa uungaji mkono wa hali na mali wa maadui wenye chuki na uhasama dhidi ya Uislamu na Waislamu, wakiongozwa na madola ya kiistikbari kama utawala wa Kizayuni na Uingereza.

Maulamaa hao wameitaka serikali ya Pakistan ichukue hatua za makusudi za kuzuia njama hizo za maadui wa Uislamu.

Wanazuoni hao wa Kiislamu wa Pakistan wameeleza kusikitishwa kwao na kitendo cha kuzalishwa filamu ya namna hiyo ambayo lengo lake si tu kuwagawanya Waislamu katika misingi ya madhehebu, lakini pia kuipaka matope dini tukufu ya Kiislamu.

Wamesema lengo la filamu hiyo ovu iliyotayarishwa na Yasser Al-Habibi ni kutaka kuchafua anga safi ya umoja, mshikamano, maelewano na udugu uliopo katika mataifa ya Kiislamu.

Wanazuoni hao wa Kishia na maulamaa wa madhehebu nyingine za Kiislamu nchini Pakistan wamesisitiza kuwa, filamu hiyo inayofahamika kwa Kiingereza kama "The Lady of Heaven" inakusudia kupanda mbegu za chuki na uhasama miongoni mwa Waislamu, ili kufikia lengo la madola ya kibeberu la kuumiza hisia na nyoyo za Umma wa Kiislamu.

Wasomi hao wa kidini wa Pakistan wamewataka Waislamu wote kote duniani, bila kujali tofauti zao za kimadhehebu kulaani kitendo hicho cha kichochezi, na kusimama kidete dhidi ya njama za maadui wa Uislamu.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni