?>

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Oman wafanya mazungumzo mjini Muscat

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Oman wafanya mazungumzo mjini Muscat

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Oman wamefanya mazungumzo ya pamoja mjini Muscat na kutilia mkazo wajibu wa kuimarishwa zaidi na zaidi uhusiano wa nchi hizi mbili ndugu.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Hossein Amir-Abdollahian na waziri mwenzake wa Oman, Sayyid Badr bin Hamad al Busaidi wamejadiliana pia masuala ya kieneo na kimataifa na njia za kuimarisha kadiri inavyowezekana uhusiano wa pande mbili.

Rais Ibrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliwasili Muscat mji mkuu wa Oman jana Jumatatu na kupokewa rasmi na Sultan Haitham bin Tariq Aal Said wa nchi hiyo.

Miongoni mwa matunda ya ziara hiyo rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Oman ni kutiwa saini hati 12 za kustawisha uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.

Jana hiyo hiyo, Iran na Oman zilitiliana saini pia hati ya pamoja ya maelewano kwa ajaili ya kutanua wigo wa ushirikiano wa kibiashara kati ya Tehran na Muscat kadiri inavyowezekana.

Hati hiyo imetiwa saini na Sayyid Reza Fatemi Amin, Waziri wa Viwanda, Madini na Biashara wa Iran na Waziri wa Biashara wa Oman, Qais bin Mohammed al Yousef.

Ziara ya Oman ni ya 5 kufanywa na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran tangu alipoingia madarakani miezi tisa iliyoopita. Msafara wa Rais Ebrahim Raisi huko Oman una mawaziri na manaibu mawaziri 50 pamoja na wakurugenzi wa ngazi za juu wa masuala ya biashara wa Iran. 

Mwaka jana, Iran na Oman zilikuwa na mabadilishano ya kibiashara yenye thamani ya dola bilioni 1.3. Sasa hivi nchi hizo mbili zinafanya juhudi za kuhakikisha mabadilishano hayo yanatanua wigo wake hadi katika masuala tofauti ya kiuchumi na kutumia vizuri zaidi fursa za uwekezaji kwa shabaha ya kuongeza zaidi na zaidi kiwango cha mabadilishano yao ya kibiashara.342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*