?>

Mazungumzo ya siri ya Marekani na Saudia; Riyadh iko mbioni kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel

Mazungumzo ya siri ya Marekani na Saudia; Riyadh iko mbioni kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel

Duru za kuaminika zinaripoti kuwa, kuna mazungumzo ya siri yanafanyika baina ya Marekani na Saudi Arabia ili kuandaa mazingira ya kuanzishwa uhusiano wa kawaida wa Riyadh na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mazungumzo hayo yanafanyika kwa usimamizi wa Rais Joe Biden wa Marekani ambaye anafanya juhudi za kuziunganisha Saudi Arabia na Israel ili zianzishe uhusiano wa kawaida baina yao.

Duru zilizoko karibu na mazungumzo hayo zinasema kuwa, endapo mazungumzo hayo yatafanikiwa, kutakuwa kumepigwa hatua moja mbele ya Saudia kuanzisha uhusiano wa kawaiida na utawala haramu wa Israel.

Watu wa karibu na mazungumzo hayo ambayo hawakutaka kutajwa majiina yao wanasema, bado hakujafikiwa mwafaka lakini mazungumzo hayo yanaendelea.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Saudi Arabia amewahi kunukuliwa huko nyuma akisema kuwa, kuanzisha uhusiano kamili wa kidiplomasia na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ni sehemu ya ndoto ya muda mrefu ya kisiasa ambayo wamekuwa nayo viongozi wa utawala wa Aal Saud.

Nchi za Kiarabu zilianza kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala wa kibaguzi wa Israel tangu Septemba 2020 kwa upatanishi au hata kwa kulazimishwa na utawala wa Doland Trump, rais wa zamani wa Marekani.

Nchi nne za Imarati, Bahrain, Morocco na Sudan zilianzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo ghasibu unaoendelea kuikaliwa kwa mabavu Quds Tukufu mwaka 2020, hatua ambayo imeendelea kulalamikiwa na Waislamu na wapenda haki.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*