?>

Mfumuko wa bei za vyakula, mgogoro wa pili kwa ukubwa UK; vikwazo vya Russia vyachangia

Mfumuko wa bei za vyakula, mgogoro wa pili kwa ukubwa UK; vikwazo vya Russia vyachangia

Matokeo ya uchunguzi wa maoni waliofanyiwa wananchi wa Uingereza yanaonesha kuwa, mfumuko wa bei za vyakula umefikia kiwango cha juu kabisa nchini humo kuliko miaka 13 iliyopita na kwamba mfumuko huo ni mgogoro wa pili kwa ukubwa huko Uingereza baada ya kupanda vibaya bei ya nishati.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa na taasisi ya kimataifa ya Kantar Worldpanel ya Uingereza yanaonesha kuwa, bei za vyakula zimepaa kwa asilimia 7 kutoka asilimia 5.9 zilivyokuwa mwezi uliopita wa Aprili.

Ripoti ya karibuni kabisa ya taasisi ya kimataifa ya kukusanya maoni iitwayo Kantar Worldpanel inaonesha kuwa, bidhaa za chakula nchini Uingereza katika wiki ya 12 inayomalizikia tarehe 15 Mei mauzo ya maduka makubwa nchini humo yamepungua kwa asilimia 4.4 ikilinganishwa na muda kama huo mwaka jana 2021.

Matokeo ya uchunguzi wa maoni waliofanyiwa wananchi wa Uingereza yanaonesha kuwa, mfumuko wa bei za vyakula umefikia kiwango cha juu kabisa nchini humo kuliko miaka 13 iliyopita na kwamba mfumuko huo ni mgogoro wa pili kwa ukubwa huko Uingereza baada ya kupanda vibaya bei ya nishati.

342/

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*