?>

Mgomo mkubwa zaidi wa reli katika miongo mitatu Uingereza, hali ya maisha ni mbaya

Mgomo mkubwa zaidi wa reli katika miongo mitatu Uingereza, hali ya maisha ni mbaya

Makumi ya maelfu ya wafanyakazi wa reli nchini Uingereza wamegoma kazi kufuatia mzozo kuhusu malipo na hali yao kazini. Mgomo huo umeifanya nchi kukwama kwani wengi hutegemea reli kwa ajili ya usafiri.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Mgomo huo wa wafanyakazi wa sekta ya reli nchini Uingereza ni mkubwa zaidi katika zaidi ya miongo mitatu.

Mgomo huo ambao utaendelea kwa siku tatu unakuja huku kukiwa na hali mbaya ya  maisha Uingereza kutokana na mfumuko mkubwa wa bei ambao sasa umepelekea kuwepo wasiwasi wa migomo zaidi nchini humo.

Wafanyakazi wa reli wamegoma baada ya mazungumzo ya mwisho ya kuepusha mgomo kuvunjika siku ya Jumatatu, huku chama cha wafanyakazi cha reli RMT kikikataa nyongeza ya mishahara ya chini ya mfumuko wa bei. Waliogoma ni wafanyakazi wa reli ya kawaida na pia reli ya chini ya ardhi au Tube  ambayo ina nafasi muhimu sana katika usafiri mjini Lodon.

Hii inamaanisha kuwa zaidi ya wanachama 50,000 wa RMT wameanza mgomo wa siku tatu yaani Jumanne, Alhamisi na Jumamosi ijayo.

Wahudumu wa reli, hata hivyo, wanaonya kuhusu kukatizwa safari kwa wiki nzima, huku njia za reli ambazo hazijaathiriwa na mgomo bado zikilazimika kupunguza huduma.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*