?>

Mgomo wa nchi nzima waanza leo Mynamar; jeshi lawatishia kifo waandamanaji

Mgomo wa nchi nzima waanza leo Mynamar; jeshi lawatishia kifo waandamanaji

Mgomo wa mamilioni ya watu umeanza leo nchini Myanmar kupinga hatua ya jeshi ya kutwaa kwa nguvu madaraka ya nchi.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mgomo huo unaotarajiwa kusimamisha kila kitu, unafanyika nchi nzima ikiwa yamepita majuma matatu tangu jeshi la Myanmar lilipotwaa madarakani ya nchi na kuwatia mbaroni viongozi wengi wa serikali ya kiraia.

Mgomo huo unakuja baada ya siku kadhaa za maandamano mtawalia ambayo yamekuwa yakikabiliwa na mkono wa chuma wa jeshi la nchi hiyo.

Wakati wananchi wa Myanmar wakiitisha mgomo wa nchi nzima, wanajeshi wanaotawala wamewataka waandamanaji kuachana na maandamano vinginevyo watapoteza maisha yao katika makabiliano na vikosi vya usalama.

Onyo hilo linakuja siku moja tu baada ya waandamanaji wawili kuuawa jana katika mji wa Mandalay moja ya miji mikubwa nchini Myanmar kufuatia kufyatuliwa risasi na vikosi vya usalama.

Itakumbukwa kuwa, tarehe Mosi ya mwezi huu wa Februari jeshi la Myanmar lilitangaza kudhibiti madaraka ya nchi baada ya kumkamata Rais wa nchi hiyo Win Myint na viongozi wengine akiwemo Aung San Suu Kyi, kiongozi wa chama tawala mwenye ushawishi nchini Myanmar, kufuatia siku kadhaa za mivutano nchini humo ambayo ilizua hofu ya kutokea mapinduzi. 

Kisingizio cha jeshi cha kufanya mapinduzi hayo ni madai ya kutokea wizi na udanganyifu katika zoezi la uchaguzi wa Bunge wa Novemba mwaka jana (2020), ambapo kwa mujibu wa matokeo, chama tawala cha National League for Democracy (NLD) kinachoongozwa na Aung San Suu Kyi kiliibuka na ushindi.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni