?>

Microsoft: Israel ndiyo iliyotuma virusi vilivyoathiri PC za Windows

Microsoft: Israel ndiyo iliyotuma virusi vilivyoathiri PC za Windows

Shirika la Microsoft linaamini kuwa, virusi vya kompyuta vilivyoathiri PC zinazotumia Windows vimetengenezwa na kusambazwa na shirika moja la utawala wa Kizayuni wa Israel.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Satya Nadella, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Microsoft amefichua hayo leo Ijumaa na kusema kuwa, shirika hilo vile vile linachunguza wadukuzi wanaosaidiwa na serikali kama taasisi ya Hafnium ya China kwani linaamini kuwa ndizo zilizohusika kushambulia mfumo wa Microsoft wa uhamishaji wa b-pepe katika sava zake.

Tatizo hilo liligunduliwa hivi karibuni tu na Microsoft na imewachukua muda mrefu kulitatua huku watu mbalimbali wakilalamika kuathiriwa na virusi hivyo, amesema, Nadella. 

Mkurugenzi huyo mtendaji wa shirika la Microsoft ameongeza kuwa, shirika lake limegundua kuwa virusi hivyo vimenezwa kampuni moja binafsi ya utawala wa Kizayuni wa Israel. 

Uchunguzi wa Microsoft unaonesha kuwa, virusi hivyo vimeenezwa na kampuni ya Israel inayoitwa Sourgum na haijajulikana lengo hasa la kufanya shambulizi hilo. 

Kundi jingine lililogunduliwa na uchunguzi wa Microsoft linajulikana kwa jina la Candiru na lina mfungamano na shirika hilo la Israel la Sourgum.

Microsoft inaamini kuwa baadhi ya wakati taasisi za mawasiliano ya Intaneti zinaeneza makusudi virusi vya compyuta ili ziweze kuuza bidhaa na programu zao za kukabiliana na virusi hivyo.

Hata hivyo kwa utawala wa Kizayuni wa Israel, ni kwamba utawala huo pandikizi hauheshimu sheria yoyote ya kimataifa na ni kawaida kwake kueneza virusi vya kompyuta kushambulioa mifumo mbalimbali ya Intaneti kwa malengo ya kufanya uharibifu na ujasusi.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*