?>

Mjadala wa kumfuta kazi Trump wafanyika katika Congress ya Marekani

Mjadala wa kumfuta kazi Trump wafanyika katika Congress ya Marekani

Congress, yaani bunge la Marekani limepasisha muswada wa kumtaka Mike Pence, Makamu wa Rais Donald Trump wa Marekani amuuzulu rais huyo ikiwa zimebaki siku sita tu kabla ya kumalizika rasmi kipindi cha utawala wake uliogubikwa na utata mwingi.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kabla ya kupasishwa muswada huo, tayari Pence alikuwa amemuandikia barua Nancy Pelosi, spika wa bunge hilo akimjulisha upinzani wake dhidi ya kuondolewa madarakani Trump kwa msingi wa marekebisho ya 25 ya katiba ya Marekani, kwa hoja kwamba hatua hiyo itaacha mfano mbaya na hatari.

Baada ya kughadhabishwa na hatua ya wahuni wanaoungwa mkono na Trump ya kuvania bunge la Congress mnamo tarehe 6 Januari, hatimaye bunge hilo linalodhibitiwa na Wademokrat, limepasisha muswada unaomtaka Pence amuuzulu Trump kwa mujibu wa marekebisho hayo ya katiba, au la, lianzishe mchakato wa kumsaili.

Muswada wa kumfukuza kazi rais huyo mwenye kiburi umejadiliwa bungeni Jumatano. Tuhuma nyingi zimetolewa dhidi ya Trump katika muswada huo ikiwa ni pamoja na kuchochea uasi dhidi ya serikali. Trump anatuhumiwa kwamba kupitia hotuba yake ya tarehe 6 Januari mbele ya White House, aliwachochea watu waliohamasishwa na hotuba hiyo kuishambulia Congress.

Seneta Mitch McConnell, Kiongozi wa waliowengi ambao ni wanachama wa chama cha Republican katika Seneti ya Marekani amesema: Trump amefanya makosa ambayo yanampasa aadhibiwe.

Kamati ya masuala ya sheria ya Congress pia imesema kuwa hotuba hiyo ya Trump iliwafanya wafuasi wake wadhani kwamba mwenendo wa demokrasia ni tishio na hivyo wakachukua hatua ya kukabiliana nao.

Iwapo bunge litathibitisha tuhuma zinazotolewa dhidi ya Trump basi atakuwa rais wa kwanza kuwahi kusailiwa mara mbili katika historia ya Marekani. Mwaka uliopita pia Trump alisailiwa bungeni kwa kushirikiana na serikali ya Ukraine dhidi ya Joe Biden, makamu wa zamani wa Marekani katika kashfa iliyotajwa kuwa Ukrainegate. Pamoja na hayo, maseneta wa Republican ambao ndio wengi kwenye Seneti waliomuondolea lawama na mashtaka yote yaliyokuwa yanamkabili kwa hoja kuwa hayakuwa na uzito wa kutosha wa kuweza kumfuta kazi.

Lakini mara hii hali ya kisiasa nchini Marekani imemlemea Trump. Kwa muda wa mwaka mmoja Trump amekuwa akikosoa na kuuponda mfumo wa uchaguzi wa Marekani na hadi kabla ya kushambuliwa Congress hakuwa tayari kukubali rasmi usahihi na uhalali wa uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo tarehe 3 Novemba mwaka uliopita. Mbali na hayo kwa kutilia maanani kuwa ni siku tano tu zimebaki kabla ya kumalizika rasmi kipindi cha utawala wa Trump hapo tarehe 20 Januari, wanachama wa Republican wanafanya kila wanaloweza kuepuka kumuondoa madarakani mwanachama mwenzao. Hii ni licha ya kuwa Marepublican pia wanamechukizwa sana na siasa za Trump na iwapo rais huyo ataamua kushiriki tena katika uchaguzi ujao wa rais bila shaka uamuazi huo utazua mfarakano na mgawanyiko mkubwa katika chama hicho.

Kwa kuzingatia suala hilo, huenda hatimaye Warepublican wakachukua uamuzi wa kupiga kura dhidi ya Donald Trump ' rais wa zamani wa Marekani' katika Seneti, hata kama tarehe ya kupigwa kura hiyo bado haijaainishwa.

342/Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni