?>

Mkurugenzi Mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu: Iran inaamiliana kwa ukarimu na wahajiri

Mkurugenzi Mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu: Iran inaamiliana kwa ukarimu na wahajiri

Mkurugenzi Mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu (ICRC) amesema kuwa kwa mtazamo wa jamii ya kimataifa Iran ni mwenyeji mzuri wa wakimbizi wa Kiafghani na inaamiliana nao kwa ukarimu.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Robert Mardini Mkurugenzi Mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu (ICRC) amekutana na kufanya mazungumzo na Pir-Hossein Kolivand Mkuu wa Shirika la Hilai Nyekundu la  Iran na kuashiria mwenendo wa ukarimu wa Iran mkabala wa wakimbizi na kuongeza kuwa kustawisha haki za binadamu kimataifa, kushirikiana katika kuwahudumia wakimbizi wa Kiafghani na kupambana na janga la UVIKO-19 ni kati ya nyanja nyingine za ushirikiano kati ya Kamati ya Kimataifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu (ICRC) na Iran. 

Mardini ameongeza kuwa: Shirika la Msalaba Mwekundu lipo tayarti kusaidia huko Yemen na Syria ilikuboresha hali ya wakimbizi na wahajiri. Amesema huko Palestina pia Kamati ya Kimataifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu inashirikiana na Iran kwa kuzingatia umuhimu wa suala hilo na kwamba shirika hilo litawasaidia raia wote walioathirika na hali ya machafuko.  

Katika mazungumzo hayo, naye Pir-Hossein Kolivand Mkuu wa Shirika la Hilali Nyekundu la Iran amesema shirika hilo lina malengo mamoja na Kamati ya Kimataifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu (ICRC) na kwamba suala hilo  linaweza kuwa na natija nzuri katika nyanja mbalimbali.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*