?>

Mkurugenzi wa wakala wa UN wa Atomiki kuitembelea Iran

Mkurugenzi wa wakala wa UN wa Atomiki kuitembelea Iran

Mkurugenzi Mkuu wa Kimataifa Nishati ya Atomiki (IAEA) anatazamiwa kuwasili Tehran leo kwa lengo la kukutana na maafisa wa ngazi za juu wa Iran.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kwa mujibu wa taarifa, Rafael Grossi Mkurugenzi Mkuu wa IAEA atakutana na Mkurugenzi wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran Mohammad Eslami. Lengo la safari hiyo limetajwa kuwa ni kujadili hali ya uhusiano wa pande mbili. 

Siku chache zilizopita, Kaimu Mwakilishi wa Iran katika taasisi za kimataifa zenye makao yao huko Vienna, Austria aliziasa nchi wanachama wa IAEA zijiepushe kutoa taarifa kwa haraka bila mazingatio juu ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.

Mohammadreza Ghayebi alitoa mwito huo Jumatano katika kikao na waandishi wa habari mjini Vienna na kuongeza kuwa, nchi wanachama wa IAEA zinapaswa kujizuia kutoa taarifa za pupa na zilizochochewa na mielekeo ya kisiasa.

Alisema wakala huo wa Umoja wa Mataifa katika ripoti yake ya hivi karibuni ulithibitisha kuwa unaendelea kufanya ukaguzi wake bila tashwishi katika vituo vya nyuklia vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Alibainisha kuwa, ripoti hiyo ya IAEA ilieleza bayana kuwa, Iran imeendelea kufungamana na majukumu yake katika kutekeleza mapatano ya nyuklia ya JCPOA.

Grossi anatembelea  Iran siku chache kabla ya kuanza mazungumzo ya Vienna yenye lengo la kufufua makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*