?>

Mkuu wa maulamaa wa Iraq: Marekani inadhamini 85% ya silaha za DAESH (ISIS)

Mkuu wa maulamaa wa Iraq: Marekani inadhamini 85% ya silaha za DAESH (ISIS)

Mkuu wa Muungano wa Maulamaa wa Kiislamu Iraq amesema, Marekani ndiyo inayodhamini asilimia 85 ya silaha za kundi la kigaidi na ukufurishaji la DAESH (ISIS).

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mwaka 2017 na baada ya mapambano ya miaka mitatu, Iraq ilitangaza ushindi dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh, lakini vikundi vidogovidogo na baadhi ya wanachama wa kundi hilo wangali wametawanyika huko na kule katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Diyala, Kirkuk, Nainawa, al Anbar na Baghdad.

Jabbar al Maamuri, Mkuu wa Muungano wa Maulamaa wa Kiislamu nchini Iraq amesema, uthabiti ndani ya nchi hiyo utapatikana kwa kuondoka askari wote wa jeshi la Marekani na maafisa wao wa kiintelijensia na akasisitiza kwamba, ushahidi na nyaraka zilizopo zinaonyesha kuwa Marekani inachukua hatua mbalimbali ili kuvuruga uthabiti na kusababisha machafuko ndani ya Iraq.

Mkuu wa Muungano wa Maulamaa wa Kiislamu Iraq ameongeza kuwa, hivi karibuni kuna watu wengi wameuliwa na wanachama wa Daesh kwa kutumia silaha mpya na za kisasa katika mikoa ya Diyala, Kirkuk na Salahuddin.

Al Maamuri amebainisha kuwa, wanachama wa Daesh wanafadhiliwa kifedha na maajinabia wa nje ya nchi, jambo ambalo linathbitika kutokana na mauaji makubwa ya halaiki ya watu wasio na hatia yanayofanywa katika baadhi ya maeneo likiwemo la Diyala.

Katika miezi ya karibuni mashambulio ya wanachama wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la DAESH (ISIS) yameshamiri katika sehemu za mashariki na kaskazini ya Iraq. Wananchi wengi na makundi mbalimbali ya nchi hiyo wanaamini kuwa kuongezeka kwa harakati za Daesh ni matokeo ya njama ya Marekani nchini Iraq inayolitumia suala hilo ili iweze kubaki na kuendelea kuikalia kwa mabavu ardhi ya nchi hiyo.../


342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*