?>

Mkuu wa Sera za Nje wa EU asisitiza ulazima wa Marekani kutumia fursa iliyopo kurudi kwenye JCPOA

Mkuu wa Sera za Nje wa EU asisitiza ulazima wa Marekani kutumia fursa iliyopo kurudi kwenye JCPOA

Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amesisitiza kuhusu ulazima wa Marekani kuitumia fursa iliyopo kwa ajili ya kurudi kwenye makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Josep Borrell, ambaye yuko mjini London, Uingereza kushiriki kikao cha mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa kundi la G7 amesema, mazungumzo muhimu kuhusu Iran yameanza pembeni ya kikao hicho na akaongeza kuwa, inapasa Marekani iitumie fursa iliyopo kwa ajili ya kurudi kwenye JCPOA.

Wakati wa utawala wa Donald Trump, Marekani ilichukua hatua ya upande mmoja ya kujitoa kwenye makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kutekeleza ugaidi wa kiuchumi kwa lengo la kuwawekea wananchi wa Iran mashinikizo ya juu kabisa.

Rais mpya wa nchi hiyo Joe Biden alikuwa mkosoaji wa sera hizo za utawala uliopita wa nchi hiyo, hata hivyo sasa anashurutisha kurudi Marekani katika JCPOA na Iran kuchukua hatua kwanza, pasi na kukiri kwanza ni nchi gani iliyotangulia kuhalifu makubaliano hayo ya nyuklia na kuamua kujitoa. Biden anadai kwamba ikiwa Iran itarudi kwenye JCPOA na kutekeleza tena kikamilifu makubaliano hayo, Washington nayo itachukua hatua ya kurudi na kutekeleza ahadi na majukumu yake.

Hata hivyo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inasisitiza kuwa, "itarudi tena kutekeleza majukumu yake katika JCPOA baada ya Marekani kuondoa kivitendo vikwazo vyote haramu ilivyoiwekea, na si kwa maneno matupu au kwa maandishi tu karatasini; na kuondolewa kwa vikwazo hivyo kupimwe na kuthibitishwa pia na Iran".../

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*