?>

Mkuu wa Sera za Nje wa EU: Hadi 2023 dunia itakuwa bado haijaishinda corona

Mkuu wa Sera za Nje wa EU: Hadi 2023 dunia itakuwa bado haijaishinda corona

Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amesisitiza kuwa utoaji chanjo ndio njia itakayowezesha kulivuka janga la corona na akatanabahisha kuwa, hadi mwaka 2023 dunia itakuwa bado haijalishinda janga hilo la maradhi ya Covid-19.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Josep Borell ameyasema hayo katika kongamano lililofanyika katika mji wa Dubrovnik, Croatia lililofanyika kwa anuani ya athari za janga la dunia nzima kwa uhusiano wa jiostratejia  na uchumi wa dunia na akaongeza kwamba, baada ya kupita mwaka mmoja na nusu tangu lilipozuka janga la dunia nzima la Covid-19 Ulaya inakaribia kulivuka janga hilo la kiafya, lakini hali ingali ngumu na mbaya huko Amerika ya Kusini, Afrika na India.

Mkuu wa Sera za Nje wa EU amebainisha kuwa, corona itaacha athari za kuwa na dunia mpya na iliyo tofauti, ya kidigitali zaidi na yenye ufa mkubwa wa kukosekana kwa usawa.

Mwanadiplomasia huyo wa Ulaya amekumbusha kuhusu indhari iliyotolewa na Umoja wa Mataifa kuhusu kukosekana njia za utoaji tiba katika baadhi ya maeneo ya ulimwengu, ikiwa na maana ya kuwepo hali tofauti za upataji nafuu wa maradhi hayo na kukosekana uthabiti kwa kiwango kikubwa zaidi; na akabainisha uungaji mkono wake kwa utoaji chanjo za misaada kwa nchi masikini ili ziweze kuimarisha maendeleo ya kiuchumi.

Tangu janga la maambukizi ya virusi vya corona lilipozuka duniani hadi sasa, zaidi ya watu milioni 187,279,000 wameambukizwa ugonjwa wa Covid-19, ambapo kati ya hao, zaidi ya milioni nne wameaga dunia na zaidi ya milioni 171 wamepata nafuu.../

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*