?>

Moscow: Siasa za Magharibi za kuingilia masuala ya ndani ya Syria hazikubaliki

Moscow: Siasa za Magharibi za kuingilia masuala ya ndani ya Syria hazikubaliki

Mwakilishi wa kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa siasa za nchi za Magharibi za kuingilia masuala ya ndani ya Syria hazikubaliki na ziinapingana na sheria za kimataifa.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Akihutubia kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Vasily Nabenza ameziusia nchi za Magharibi kukomesha propaganda chafu kuhusiana na uchaguzi wa rais nchini Syria na kuacha kuingilia masuala ya nchi ya nchi hiyo. 

Vasily Nabenza amesema kuwa, licha ya matatizo na changamoto nyingi zilizopo, serikali ya Syria imechukua hatua za dharura za kuhakikisha kuwa mfumo wa serikali unafanya kazi kwa ufanisi. Ameongeza kuwa, inasikitisha kuona baadhi ya nchi zikipinga suala la kuitishwa uchaguzi wa rais nchini Syria na tangu sasa zinautaja kuwa si halali. Mwakilishi huyo wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema msimamo kama huo haukubali. 

Vasily Nabenza amesisitiza kuwa, Russia inatarajia kuwa nchi zote zitakomesha propaganda chafu kuhusiana na uchaguzi ujao nchini Syria. 

Uchaguzi wa rais wa Syria umepangwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu wa Mei. Hadi sasa wagombea 51 akiwemo rais wa sasa wa nchi hiyo, Bashar Assad, wanawania nafasi hiyo.    

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*