?>

Mpango wa Muamala wa Karne, utawala wa Saudia mfuasi bubu na kipofu wa Marekani

Mpango wa Muamala wa Karne, utawala wa Saudia mfuasi bubu na kipofu wa Marekani

Msimamo uliotangazwa na maafisa wawili wa ngazi za juu wa utawala wa Saudi Arabia kuhusu Iran na mpango wa Kimarekani uliopewa jina la “Muamala wa Karne” umeonesha tena kwamba, baadhi ya tawala za Kiarabu zinashirikiana na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel katika utekelezaji wa mpango huo khabithi na katika kufanya mabadiliko kwenye eneo la magharibi mwa Asia.

(ABNA24.com) Alkhamisi iliyopita Waziri Mshauri katika Masuala ya Nje wa Saudia, Adel al Jubeir alidai kuwa, mpango wa Muamala wa Karne uliopendekezwa na Donald Trump una vipengee chanya na unaweza kutumiwa kama msingi wa kuanza mazungumzo. Wakati huo huo Wazizi wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Faisal bin Farhan Al Saud alisema kuwa sharti na kuwepo uhusiano baina ya Waarabu na Israel ni kupatikama njia ya ufumbuzi itakayokubaliwa na kudai kuwa, Iran ni adui wa pande zote.

Misimamo hiyo miwili ya maafisa wa ngazi za juu wa serikali ya kifalme ya Saudia ni kielelezo kwamba, baadhi ya tawala za Kiarabu hususan utawala wa ukoo wa Aal Saud zinafanya mikakati ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel, adui nambari moja wa Waarabu na Umma wa Kiislamu.

Hatua ya kwanza kabisa ya utekelezaji wa njama hiyo iliyopewa jina la Muamala wa Karne ya Marekani na Wazayuni dhidi ya taifa la Palestina na Umma ni kuwepo ushirikiano wa baadhi ya tawala za Kiarabu na ili katika hatua ya pili malengo ya Trump na Netanyahu yatimizwe na kutekelezwa.

Iran na kambi ya maambano na muqawama ni vizingiti viwili vikubwa katika njia ya utekelezaji wa mpango na njama hiyo ya Kiarabu na Kiyahudi katika eneo la Magharibi mwa Asia; kwa sababu hiyo Wamarekani na vibaraka wao wa kikanda kama utawala wa Riyadh wanafanya harakati ya kisiasa na kipropaganda za kuhujumu Iran kwa shabaha ya kufanikisha njama hiyo.

Katika fremu hiyo Marekani inafanya kila iwezalo kuiarifisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni adui mkubwa na utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa ni rafiki wa nchi za kanda hiyo. Propaganda hii inatumia vyombo vya habari kuhubiri na "kuuza" mpango wa Muamala wa Karne katika nchi za magharibi mwa Asia na Umma wa Kiislamu.

Katika mazingira kama haya kuna udharura wa kuuzinda Umma kuhusiana na njama iliyopewa jina la Muamala wa Karne. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, watu wanajua kwamba Jamhuri ya Kiislamu daima imekuwa mstari wa mbele katika kuwatetea Wapalestina na inafanya jitihada kubwa za kuhakikisha wanapata haki zao zote. Baada tu ya kuzinduliwa mpango huo wa Kizayuni, Iran ilitangaza kuwa, iko tayari kufanya mazungumzo na nchi zote za Kiislamu na Kiarabu ili kubatilisha malengo ya mpango na njama hiyo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Sayyid Abbas Mousavi amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu iko tayari kufanya mazungumzo na nchi zote za Kiislamu katika nyanja zote kwa ajili ya kukabiliana na njama ya karne na kuongeza kuwa: “Kuna njama kubwa inayojificha nyuma ya kile kinachoitwa “Muamala wa Karne”.

Malengo ya mpango huo khabithi yanakwenda zaidi ya jiografia ya Palestina na kulenga maeneo mengine ya Waarabu na Waislamu; hivyo mghafala wowote katika uwanja huu utakuwa na taathira mbaya sana kwa nchi zote za Kiarabu hususan Saudi Arabia ambayo kwa kujua au kutojua itajikutaka ikisombwa na mawimbi ya njama hiyo.

Baada ya kudhihirika wazi athari mbaya na hatari ya mpango huo wa Kizarekani-Kizayuni, sasa inaonekana kuwa mpango wa “Muamala wa Karne” utaendelea kuwa ndoto na njozi tupu katika akili na bongo za wale walioubuni na vibaraka wao wa akikanda hususan Saudi Arabia.

............
340


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni