?>

Mtawala kijeshi Myanmar awa Waziri Mkuu na kuahidi uchaguzi mkuu 2023

Mtawala kijeshi Myanmar awa Waziri Mkuu na kuahidi uchaguzi mkuu 2023

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Ulinzi ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza jipya la Utawala la Taifa nchini Myanmar Min Aung Hlaing amechukua jukumu la uwaziri mkuu katika serikali mpya ya mpito na kuahidi kuandaa uchaguzi mpya ifikapo mwaka 2023.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Tangazo hili linatolewa miezi sita baada ya jeshi la Myanmar kutwaa madaraka ya nchi baada ya mapinduzi ya kijeshi ya Februari Mosi mwaka huu.

Min Aung Hlaing ameongoza Baraza la Utawala la kitaifa (SAC) lililoundwa baada ya mapinduzi na limekuwa likitawala Myanmar tangu wakati huo, na sasa serikali ya muda itachukua nafasi ya baraza hilo.

Min Aung Hlaing amesema kuwa Myanmar inatarajia kufanya uchaguzi mkuu mpya katika nusu ya pili ya mwaka 2023 ambayo itakuwa Agosti, baada ya kufanya maandalizi kwa miezi sita.

Kamanda Min Aung Hlaing pia ameahidi kufanya uchaguzi mkuu wa vyama vingi, akisisitiza haja ya kuweka mazingira ya kufanyika uchaguzi mkuu ulio huru na wa haki na kuvishirikisha vyama vyote vya kisiasa.

Jeshi la Myanmar lilitwaa madaraka ya nchi Februari Mosi mwaka huu baada ya kumkamata Rais wa nchi hiyo, Win Myint na viongozi wengine akiwemo Aung San Suu Kyi, kiongozi wa chama tawala mwenye ushawishi mkubwa, kufuatia siku kadhaa za mivutano nchini humo.

Kisingizio cha jeshi cha kufanya mapinduzi hayo ni madai yake ya kutokea wizi na udanganyifu katika zoezi la uchaguzi wa Bunge wa Novemba mwaka jana (2020), ambapo kwa mujibu wa matokeo, chama tawala cha National League for Democracy (NLD) kinachoongozwa na Aung San Suu Kyi kiliibuka na ushindi.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*