?>

Mufti wa Oman: Katika mwezi huu wa Ramadhani, Waislamu wasiisahau Quds, Masjidul Aqsa na Gaza

Mufti wa Oman: Katika mwezi huu wa Ramadhani, Waislamu wasiisahau Quds, Masjidul Aqsa na Gaza

Mufti wa Oman Sheikh Ahmed bin Hamad al Khalili amesisitiza kuwa katika masiku ya mwezi huu wa Ramadhani Waislamu wasiisahau Quds, Msikiti wa Al Aqsa na Gaza.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Sheikh Al-Khalili ameandika katika ukurasa wake wa Twitter: "Katika masiku ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, ambapo milango ya mbinguni hufunguliwa na dua kutakabaliwa, Waislamu wasiwasahau ndugu zao mashujaa walioko Quds ambao wanailinda haram tukufu ya Baitul Muqaddas."

Aidha Mufti wa Oman amewataka Waislamu wawaombee dua na kuwapa msaada mashujaa wa jihadi na mapambano katika Ukanda wa Gaza ambao mithili ya mlima, wamesimama imara na kwa umoja kukabiliana na utawala ghasibu.

Kwa muda wa zaidi ya wiki moja sasa Quds imekuwa uwanja wa hujuma na ukandamizaji mkali unaofanywa na askari wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina ambao wamefanya mgomo wa kuketi katika uwanja wa Babul-a'muud wa Msikiti wa Al Aqsa kuonyesha upinzani wao dhidi ya usambazwaji wa askari wa Kizayuni katika eneo hilo kwa lengo la kuugawanya utumiaji wa msikiti wa Al Aqsa kieneo na kiwakati.../

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*