?>

Muqawama; njia pekee ya kukabiliana na utawala ghasibu wa Kizayuni

Muqawama; njia pekee ya kukabiliana na utawala ghasibu wa Kizayuni

Viongozi wa makundi ya kupigania ukombozi wa Palestina pamoja na wananchi wamesisitiza kuwa njia pekee ya kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel ni muqawama au mapambano.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA:Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Utawala wa Kizayuni wa Israel na Benny Gantz mkuu wa chama cha Buluu na Nyeupe mwisoni mwa mwezi Aprili waliafikiana kuhusu oparesheni ya kupora maeneo makubwa ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kuanzia Julai Mosi.

Uchunguzi umebaini kuwa Wazayuni wanalenga kupora asilimia 30 ya ardhi zote za Ukingo wa Magharibi. Mapatano hayo ya Netanyahu na Gantz ni sehemu ya mpango wa kibaguzi wa 'Muamala wa Karne' ambao ulizinduliwa Januari 28 na Rais Donald Trump wa Marekani.

Wananchi na viongozi wa makundi ya muqawama au wapigania ukombozi wa Palestina walitangaza tokea awali kuwa wanapinga 'Muamala wa Karne' kwa sababu muamala huo unaenda sambamba na maslahi ya utawala wa Kizayuni na wakati huo huo kukinzana kikamilifu na maslahi ya Palestina. Mbali na kuwa muamala huo unadhoofisha misingi ya kujihami ya Wapalestina, pia umepunguza kwa kiasi kukubwa ardhi ambazo Palestina ilikuwa imesalia nazo. Hivi sasa Netanyahu na Gantz wameafikiana kuwa, eneo kubwa la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan litaunganishwa na ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel).

Wapalestina ambao wameitaka jamii ya kimataifa kukabiliana na hatua za kijinai za utawala wa Kizayuni wa Israel, wanasisitiza kuliko wakati mwingine wowote kuwa, mapambano au muqawama ndio njia pekee ya kukabiliana na utawala dhalimu wa Israel.

Kuhusiana na nukta hii, Ashraf Zaid mkuu wa Idara ya Wananchi katika Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesisitiza kuhusu ulazima wa kuimarisha umoja wa kitaifa baina ya Wapalestina. Ameongeza kuwa, njia pekee ya kukabiliana na njama za Wazayuni ni muqawama na mapambano. Naye msemaji wa Harakati ya Jihad Islami Musab al-Berim anasema pamoja na kuwepo ukandamizaji unaotekelezwa na Wazayuni katika Ukingo wa Magharibi lakini taifa la Palestina halitashindwa katika mapambano hata kama ni mawe pekee yatakayosalia kama silaha ya mapambano.

Muqawama au mapambano ni mbinu ambayo ina muelekeo wa wananchi wa kawaida na pia mueleko wa kijeshi. Muelekeo wa wananchi katika muqawama unadhihirika katika kutumia mawe kama silaha na kujitolea katika oparesheni za kufa shahidi. Kuhusiana na nukta hii, Jeshi la Utawala wa Kizayuni limetangaza kuwa askari wa utawala huo ambaye alikuwa ameenda katika kijiji cha Yaid cha Jenin kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi aliuawa baada ya kupigwa kwa mawe na Wapalestina. Aidha kijana Mpalestina alifika karibu na kituo cha upekuzi cha Qalandiya kaskazini mwa Quds (Jerusalem) akiwa na nia ya kutekekeleza oparesheni ya kufa shahidi dhidi ya Wazayuni lakini alifyatuliwa risasi na kukamatwa na askari wa Israel.

Muelekeo wa kijeshi wa muqawama na mapambano unatumiwa na makundi ya kisiasa hasa makundi ya kimuqawama kama vile Hamas na Jihad Islami. Katika kipindi cha miezi 18 iliyopita, makundi ya muqawama yametoa jibu kali kwa jinai za kutawala wa Kizayuni na kuusababishia utawala huo hasara kubwa za kijeshi. Aidha hivi sasa kipindi cha utawala wa Kizayuni kustahamili vita dhidi ya makundi ya muqawama ya Palestina kimepungua hadi siku mbili tu. Hivi sasa makundi ya muqawama ya Palestina yameuonya vikali utawala wa Kizayuni kuwa, yatakabiliana vikali na mipango ya utawala huo wa Kizayuni ya kujitanua na kupora ardhi zaidi za Palestina.

Nukta muhimu katika harakati za muqawama huko Palestina ni kuwa hazitegemei msaada wa kijeshi kutoka nje. Makundi ya muqawama na kupigania ukombozi wa Palestina yanategemea uwezo wa ndani na hivyo yameweza kuimarisha nguvu za kukabiliana na utawala huo.

Muelekeo huu pia umetumiwa katika kukabiliana na muungano wa kivita wa Saudia dhidi ya Yemen ambapo, kamati za wananchi wa Wayemen zimefanikiwa kutoa pigo kubwa kwa Saudia na vibaraka wake.

Hivi sasa pia wananchi wa Palestina kwa kushirikiana na makundi ya muqawama wataweza kuzuia kutekelezwa mpango hatari wa utawala bandia wa Israel ambao unalenga kupora ardhi zaidi za Wapalestina.

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni