?>

Muqawama Palestina waionya Israel, waitaka isijifungulie milango ya jahanamu

Muqawama Palestina waionya Israel, waitaka isijifungulie milango ya jahanamu

Makundi ya mapambano huko Palestina yameuonya utawala haramu wa Israel na kuutaka usithubutu kuchukua hatua yoyote ya kijinga ya kuwaua viongozi wa muqawama kwani kufanya hivyo ni kujifungulia milango ya jahanamu.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mushir al-Masri, mjumbe mwanadamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema, endapo utawala haramu wa Israel utachukkua hatua ya kumuua Yahya Sinwar au kamanda mwingine yeyote wa muqawama utakuwa umetoa muhanga mustakabali wake.

Kiongozi huyo mwandamizi wa HAMAS amesisitiza kuwa, tutaendeleza njia yetu ya muqawama kwa ushindi au kwa kuuawa shahidi na katu hatuzingatii au kuvipatia umuhimu vitisho vya utawala ghasibu wa Israel.

Msimamo huo wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) na makundi mengine ya Palestina unatolewa baada ya kiongozi mmoja baada ya mwingine wa utawala ghasibu wa Israel kunukuliwa akitoa vitisho vya kutaka kuuawa viongozi wa muqawama huko Palestina akiwemo Yahya Sinwar.

Hivi karibuni Wapalestina walitekeleza operesheni nyingine katika kitongoji cha walowezi cha El'ad huko Mashariki mwa Tel Aviv ambapo wazayuni watatu waliangamizwa na wengine wanne wamejeruhiwa.

Maafisa wa Kizayuni wa Israel wamembebesha lawama za operesheni hiyo Yahya Sinwar ambaye ni miongoni mwa maafisa wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) na wametoa wito wa kuuawa kwake.

Katika hotuba yake kwenye maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds kwenye Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani, Sinwar alipongeza operesheni za Wapalestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*