?>

Muungano vamizi wa Saudi Arabia washambulia maeneo mbalimbali ya Yemen

Muungano vamizi wa Saudi Arabia washambulia maeneo mbalimbali ya Yemen

Ndege za kijeshi za muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia zimefanya hujuma na mashambulio ya anga dhidi ya maeneo mbalimbali ya Yemen.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ripoti kutoka Yemjen zinasema kuwa, jana ndege za kivita za muuungano vamizi wa Saudi Arabia zimefanya mashambulio mara  nane katika mji wa Sarwah na mara sita dhidi ya mji wa al-Jawbah katika mkoa wa Ma'rib.

Aidha miji mingine kadhaa ya Yemen jana iliandamwa kwa mashambulio ya mabomu ya muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia ukiwemo mkoa wa Sa'da na Uwanja wa Ndege wa Taizz.

Watu kadhaa wanaripotiwa kuuawa na kujeruhiwa katika mashambulio hayo huku kukishuhudiwa uharibu mkubwa wa nyumba na mali za watu.

Hujuma na mashambulio hayo ya Saudia na washirika wake yanaendelea licha ya kuweko miito ya kieneo na kimataifa inayotaka kusitishwa mauaji hayo dhidi ya wananchi wa Yemen.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*