?>

Mwana wa kiume wa Muammar Gaddafi akataliwa kugombea urais

Mwana wa kiume wa Muammar Gaddafi akataliwa kugombea urais

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Libya imewakatalia shakhsia 25 akiwemo Saiful Islam Gaddafi mwana wa kiume wa kiongozi wa zamani wa Libya Kanali Muammar Gaddafi kugombea uchaguzi ujao wa rais nchini humo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Libya jana pia ilitangaza kuwa imethibitisha katika orodha ya kwanza  majina ya watu 73 wanaostahiki kushiriki uchaguzi wa rais akiwemo Khalifa Haftar Kamanda wa kundi la wanamgambo kwa jina la jeshi la kitaifa la Libya.  

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, katika orodha hiyo ya majina ya wagombea 73 waliothibitishwa yanaonekana majina ya shakhsiya kama Abdul Majid Dbeibeh Waziri Mkuu wa serikali ya Libya, Aguilah Saleh Spika wa Bunge na Fathi Bashaga Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo. 

Saiful Islam Gaddafi anasakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kwa kushiriki katika mauaji wakati wa vuguvugu la kuikomboa nchi hiyo katika maandamano ya mwaka 2011 yaliyomuangusha madarakani baba yake mwendazake Muammar Gaddafi. Itakumbukwa kuwa mahakama katika mji wa Zanten ilimhukumu kunyongwa mwana huyo wa kiume wa Gaddafi, Saiful Islam Gaddafi. 

Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Libya imeeleza kuwa  shakhsia waliokataliwa kugombea kiti cha urais wana muda wa siku 12 kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo. Jumla ya wagombea 98 walijiandikisha kwa ajili ya uchaguzi ujao wa rais huko Libya. Uchaguzi wa rais na bunge Libya umepangwa kufanyika Disemba 24 mwaka huu licha ya makundi na taasisi mbalimbali nchini humo kuhitilafiana kuhusu sheria za uchaguzi. 342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*