?>

Mwanafalsafa mtajika wa Ujerumani akataa tuzo ya kifahari ya UAE

Mwanafalsafa mtajika wa Ujerumani akataa tuzo ya kifahari ya UAE

Msomi na mwanafalsafa mashuhuri wa Ujerumani amekataa kupokea tuzo ya kifahari ya uandishi wa vitabu kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu kutokana na kile kinachoonekana ni kutoafiki mfumo wa kisiasa wa nchi hiyo ya Kiarabu na historia yake ya ukiukaji wa haki za binadamu.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kwa mujibu wa shirika la habari la mtandaoni la Spiegel, mwanafalsafa Juergen Habermas ameghairisha msimamo wake wa awali wa kukubali kupokea tuzo hiyo ya kazi za fasihi ya 'Sheikh Zayed Book Award', baada ya kugundua kuwa watoaji wa tuzo hiyo wana mfungamano wa moja kwa moja na mfumo wa kisiasa wa Imarati.

Habermas mwenye umri wa miaka 91 amesema katika taarifa kuwa, "Nilitangaza azma yangu ya kukubali kupokea tuzo ya mwaka huu ya Sheikh Zayed. Huo ulikuwa uamuzi ghalati, ambao nausahihisha sasa."

Mwandishi huyo mashuhuri wa zama hizi za Ujerumani amebainisha kuwa, anasikitika kwa kutogundua ukuruba wa taasisi inayotoa tuzo hiyo mjini Abu Dhabi na mfumo wa kisiasa wa nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi.

Watoaji wa tuzo hiyo walikuwa wamemtaja Habermas kama 'Shakhsia wa Utamaduni wa Mwaka 2021' na kumteua kwa tuzo hiyo ya kifahari kutokana na mchango wake mkubwa katika tasnia ya uandishi wa vitabu, kwa zaidi ya nusu karne. Mshindi wa tuzo hiyo hutunukiwa Dirham milioni moja za UAE (Dola 272,249 za Marekani).

Imarati imekuwa ikikosolewa kutokana na rekodi yake ya kukiuka haki za binadamu, mbali na faili jeusi la kuwa mshirika mkuu wa muungano vamizi wa Saudia unaomwaga damu za wananchi wa Yemen tokea Machi mwaka 2015.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*