?>

Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah atilia mkazo umuhimu wa Siku ya Kimataifa ya Quds

Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah atilia mkazo umuhimu wa Siku ya Kimataifa ya Quds

Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema, baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran uliopatikana kwa uongozi wa Imam Khomeini (MA), kiongozi huyo alisema, Siku ya Quds ni siku ya Uislamu na Siku ya Walionyongeshwa duniani.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Sheikh Naim Qassem amebainisha kuwa, baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu tumeingia katika zama mpya ambazo ni zama za muqawama wa kukabiliana na adui Israel; na muqawama huo umejengeka katika eneo zima la Asia Magharibi.

Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ameeleza pia kwamba, kwa mshikamano na ushirikiano wake, muqawama umethibitisha kuwa, unao uwezo wa kutoa matunda muhimu kwa ajili ya kufanikisha lengo la ukombozi wa Quds na akaongeza kuwa, kaulimbiu ya "Quds i karibu mno" ni nara inayowapa matumaini makubwa zaidi mujahidina na wananchi.

Kwa ubunifu wa Imam Ruhullah Khomeini (MA), mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani imepewa jina la Siku ya Kimataifa ya Quds.

Maandamano ya mwaka huu ya Siku ya Kimataifa ya Quds yatafanyika Ijumaa ya tarehe 7 Mei katika nchi nyingi duniani.../

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*