?>

Nasrallah aionya Israel: "Acheni kucheza na moto"

Nasrallah aionya Israel:

Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameuonya vikali utawala wa Kizayuni wa Israel na kuutaka kutocheza na moto huku akisisitiza kuwa hujuma yoyote ile ya Israel dhidi ya Lebanon itakabiliwa na jibu kali kutoka kwa Hizbullah.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Sayyid Hassan Nasrallah ameyasema hayo katika hotuba ya Televisheni Jumanne usiku kwa mnasaba wa kukumbuka kuuawa shahidi makamanda wa ngazi za juu wa Hizbullah akiwemo Shahidi Imad Mughniyeh ambaye aliuawa Syria mnamo Februari 2008.

Sayyid Nasrallah amesema Hizbullah haitaki makabiliano ya kijeshi lakini itapambana kwa nguvu zaidi kuliko miaka ya nyuma iwapo italazimishwa kuingia vitani. Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema utawala haramu wa Israel katu haujawahi kufungamana na sheria za kimataifa na huharibu miji na kuua raia katika vita vyake vyote.

Katika hotuba yake, Katibu Mkuu wa Hizbullah amepongeza 'hatua chanya' iliyochukuliwa na Marekani ya kuacha kuunga mkono hujuma ya Saudia dhidi ya Yemen. Sayyid Nasrallah amesema uamuzi huo umetokana na kusimama kidete Wayemeni.

Katibu Mkuu wa Hizbullah pia amekosoa mapatano ya nchi chache za Kiarabu na utawala wa Kizayuni wa Israel na kusema utawala wa Kizayuni umekuza kupita kiasi mapatano hayo kwa maslahi ya kisiasa.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake Kiongozi wa Hizbullah amesema leo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni dola lenye nguvu na uwezo mkubwa katika eneo la Asia Magharibi. Amesema Iran imeweza kusimama kidete mbele ya mashinikizo na vikwazo vya Marekani na waitifaki wake.

Kuhusiana na mwamako wa wananchi wa Bahrain dhidi ya utawala wa ukoo wa Aal Khalifa, Sayyid Nasrallah amesema Wabahrain wakiongozwa na Sheikh Issa Qassim wamejitolea muhanga kwa ajili ya uhuru.


342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni