?>

Nasrullah: Daesh ilianzishwa ili kuwasahaulisha Waislamu kadhia ya Palestina

Nasrullah: Daesh ilianzishwa ili kuwasahaulisha Waislamu kadhia ya Palestina

Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa moja kati ya malengo ya kuanzishwa kundi la kigaidi la Daesh ni kuwasahaulisha Waislamu kadhia ya ukombozi wa Palestina.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Sayyid Hassan Nasrullah ambaye alikuwa akizungumza jana katika ufunguzi wa mkutano wa "Palestina Itashinda", amesema kuwa, mashambulizi yoyote yanayofanywa na Israel huwa ni mashambulizi ya Marekani, na kwamba udhibiti na ubeberu wa Marekani ni tishio kubwa zaidi kwa watu wa eneo la Magharibi mwa Asia hususan Iraq na Syria; hivyo watu wa eneo hilo wana haki ya kujiainishia mambo yao wenyewe.

Sayyid Nasrullah amesema kuwa, vyombo vya habari ni moja kati ya nyenzo muhimu za kukabiliana na adui na kwamba kusimama kidete kambi ya muqawama na mapambano ni miongoni mwa mambo yaliyochangia katika ushindi wa karibuni wa Wapalestina katika Operesheni ya Panga la Quds.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema kambi ya muqawama imeahidi kuikomboa Quds na hapana shaka kwamba itatekeleza ahadi yake.  

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*