?>

Nchi 8 za Afrika miongoni mwa 39 duniani zilizoripoti Monkeypox

Nchi 8 za Afrika miongoni mwa 39 duniani zilizoripoti Monkeypox

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema nchi 8 za Afrika ni miongoni mwa nchi 39 duniani zilizoripoti kesi zilizothibitishwa za ugonjwa wa Monkeypox.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Dakta Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa kieneo wa WHO barani Afrika amesema watu 1,200 katika nchi 39 duniani wamethibitishwa kuambukizwa ugonjwa huo wa virusi hadi kufikia sasa.

Amesema nchi sita kati ya nane za Kiafrika zilizoripoti kesi mpya za maradhi hayo ya kuambukiza, zimewahi kuripoti visa vya ugonjwa huo katika miaka ya nyuma.

Dakta Moeti amesema Nigeria ndiyo inayoongoza barani Afrika kwa kuwa na kesi nyingi za maradhi hayo, na kwamba hadi sasa taifa hilo la Afrika Magharibi limeripoti kesi 36, likifuatia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo-kesi 10, huku Benin ikishika nafasi ya tatu barani kwa kunakili kesi 8.

Mkurugenzi wa kieneo wa WHO barani Afrika amefafanua kuwa, nchi mbili za Afrika ambazo hazina historia ya kusajili kesi za mara hayo huko nyuma ni Ghana, ambayo hivi sasa imerekodi kesi 5 na Morocco kesi moja.

Fauka ya hayo, amesema mataifa saba ya Kiafrika ambayo hayajawahi kuripoti kesi za ugonjwa wa Monkeypox lakini hivi sasa kuna kesi zinazoshukiwa kuwa za maradhi hayo ni Ethiopia, Guinea, Liberia, Msumbiji, Sierra Leone, Sudan na Uganda.

Kesi ya kwanza ya ugonjwa huu iliripotiwa kwa mara ya kwanza huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika muongo wa 70 na kuenea kutoka mnyama hadi kwa mwanadamu baada ya kukaribiana.342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*