?>

Nchi za Ulaya kuisaidia Misri kukabiliana na makali ya mgogoro wa Ukraine

Nchi za Ulaya kuisaidia Misri kukabiliana na makali ya mgogoro wa Ukraine

Misri imepata msukumo mpya katika juhudi zake za kupata za usalama wa chakula baada ya Umoja wa Ulaya kuahidi kuipa nchi hiyo ya kaskaizni mwa Afrika, msaada wa euro milioni 100 (dola milioni 104 za Kimarekani) ili kusaidia raia hasa wakulima kukabiliana na makali ya maisha yaliyosababishwa hasa na mgogoro wa Ukraine.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Bi Ursula von der Leyen amesema hayo akiwa pamoja na Rais Abdel Fattah el Sisi wa Misri na kuongeza kuwa, EU itatoa msaada wa haraka wa euro milioni 100 kwa Misri ili kushughulikia haraka mgogoro wa chakula unaozidi kuwa mkubwa nchini humo. Amesema, fedha hizo zimepangiwa kutumika kwa ajili ya kukabiliana na nakisi kubwa ya nafaka na pia kusaidia wafanyabiashara wa vijijini na wakulima.

Von der Leyen amedokeza kwamba hiyo itakuwa ni hatua ya muda mfupi tu na kwamba nchi hiyo ya Afrika Kaskazini italazimika kuongeza uzalishaji wake wa chakula wa ndani kwa ajili ya kuwa na usalama wa chakula wa muda wa kati na wa muda mrefu na pia kuiwezesha Misri kupunguza kutegemea maeneo mengine.

Hayo yameripotiwa katika hali ambayo hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia alisema wakati anajibu swali la mwandishi wa habari wa serikali ya Ukraine akiwa pamoja na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Uturuki, Mevlüt Çavuşoğlu, kwamba Moscow imekuwa ikitangaza muda wote kuwa haina kizuizi chochote cha kusafirishwa bidhaa muhimu zikiwemo za nafaka nje ya Ukraine. Alisema, kinachosubiriwa na Russia ni ruhusa kutoka kwa rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy ili bidhaa za nchi hiyo ziweze kupelekwa nja ya Ukraine.

Hata hivyo Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia alisema, anaamini kuwa, uamuzi hauko kwa rais wa Ukraine, bali unatolewa na madola ya Magharibi na ndiyo yanayokwamisha kuwafikia walimwengu bidhaa muhimu zilizokwama huko Ukraine.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*