?>

Nebenzia: Dunia imo katika vita vya kiuchumi vya dunia

Nebenzia: Dunia imo katika vita vya kiuchumi vya dunia

Balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa vita vya dunia katika upeo wa kiuchumi vinaendelea sasa dhidi ya Russia kwa ajili ya kukabiliana na operesheni maalumu ya kijeshi ya Russia nchini Ukraine.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Vasily Nebenzia aliyekuwa akihutubia mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Ukraine amezituhumu nchi za Magharibi kwamba zimekataa mapendekezo yote ya Russia kuhusu wasiwasi wake juu ya kupanuliwa Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) upande wa Mashariki na kusema: Wamagharibi walikuwa wakisubiri vita hii ili waanze kuisambaratisha nchi ya Russia.

Nebenzia ameongeza kuwa, ukubwa na kasi ya vita vya kiuchumi vya Marekani na Ulaya dhidi ya Russia inaonyesha kuwa nchi za Magharibi zimejiandaa kwa vita vya muda mrefu dhidi ya Russia.

Mwakilishi wa kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa: "Kinyume na inavyotangazwa, hivi sio vita vya Ukraine, hivi ni vita vya niaba vya nchi za Magharibi dhidi ya Shirikisho la Russia." 

Rais Vladimir Putin wa Russia tarehe 24 Februari alitangaza kuanza operesheni maalumu ya kijeshi nchini Ukraine baada ya viongozi wa maeneo yaliyojitangazia uhuru ya Donetsk na Luhansk huko mashariki ya Ukraine kuiomba Russia iwatumie misaada ya kijeshi kwa mujibu wa makubaliano ya ushirikiano kati yao. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*