?>

Ofisi ya Sheikh Zakzaky: Israel ni COVID ya mwaka 1948

Ofisi ya Sheikh Zakzaky: Israel ni COVID ya mwaka 1948

Ofisi ya Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imetoa ujumbe kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuasisiwa utawala pandikizi wa Kizayuni uliopachikwa jina bandia katika ardhi walizoporwa Wapalestina na kusema kuwa, Israel ni "COVID-1948."

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA:Mwandishi wa shirika la habari la IRIB amenukuu taarifa ya ofisi ya Sheikh Ibrahim Zakzaky anayeshikiliwa kidhulma katika jela za Nigeria ikisema kwa mnasaba wa siku ya "Nakba" ya kupandikizwa utawala wa Kizayuni wa Israel katika ardhi walizoporwa Wapalestina mwaka 1948 watoto wa kaskazini mashariki mwa Nigeria wameonesha mshikamano wao na taifa linalodhulumiwa la Palestina katika kumbukumbu ya siku ya "Nakba" na wamepandisha juu bendera ya Palestina kama njia ya kutangaza hasira zao kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katika ujumbe huo, ofisi ya Sheikh Zakzaky imeweka picha inayoonesha bendera ya Palestina ikipepea huko kaskazini mashariki mwa Nigeria na kuandika: Utawala haramu wa Israel ni COVID-1948.

Jana na juzi yaani Alkhamisi na Ijumaa tarehe 14 na 15 Mei zilisadifia na kuingia mwaka wa 72 wa kuporwa na kufukuzwa mamia ya maelefu ya Wapalestina katika ardhi zao na kupandikizwa utawala dhalimu uliopachikwa jina la Israel katika ardhi za Wapalestina hao.

Kila ikifika tarehe 15 Mei, wananchi wa Palestina huwa wanafanya kumbukumbu za siku ya "Nakba" yaani siku ya nakama ya kupandikizwa utawala haramu wa Israel kwenye ardhi zao.
Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni