?>

OIC, nchi za Kiislamu zinalaani uchokozi wa walowezi wa Israeli dhidi ya Msikiti wa al-Aqsa

OIC, nchi za Kiislamu zinalaani uchokozi wa walowezi wa Israeli dhidi ya Msikiti wa al-Aqsa

Jumuiya ya la Ushirikiano wa Kiislamu (OIC), mataifa ya Kiislamu na harakati za mapambano ya ukombozi wa Palestina wamelaani vikali hatua ya vikosi vya jeshi la utawala haramu wa Israei ya kuvunjia heshima viwanja vya Msikiti wa al-Aqsa huko Mashariki la al-Quds inayokaliwa kwa mabavu, na kuwaruhusu walowezi wenye itikadi kali kuwashambulia Waislamu waliokuwa wakifanya ibada katika eneo hilo tukufu.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Taarifa iliyotolewa na OIC imesema kwamba hujuma hiyo ni sehemu ya mradi wa serikali ya Tel Aviv wa kubadilisha hali ya kihistoria na kisheria ya al-Quds, ikisisitiza kuwa majaribio kama hayo ni ukiukaji wa sheria za kimataifa, Mkataba wa Geneva na maazimio ya Umoja wa Mataifa.

Jumuiya hiyo imeubebesha utawala ghasibu wa Israeli athari mbaya za matokeo ya mashambulio hayo ya kimfumo, ikitoa wito kwa jamii ya kimataifa, haswa Baraza la Usalama la UN, kutekeleza majukumu yake na kukomesha uhalifu huo.

Wakati huo huo semaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya Misri Ahmed Hafez ameshutumu hujuma iliofanywa na walowezi wenye itikadi kali chini ya ulinzi wa polisi wa Israeli huko al Aqsa na kutoa wito wa kujiepusha na harakati yoyote inayoweza kuvuruga amani.

Jumatatu ya jana sambamba na maadhimisho ya Siku ya Arafa huko Palestina, makumi ya walowezi wa Kizayuni waliokuwa wakipewa himaya na ulinzi wa polisi ya Israel walivamia tena viwanja vya Msikiti wa al Aqsa na kuwashambulia Wapalestina waliokuwa ndani ya msikiti huo. 

Askari wa Israel pia waliwalazimisha Waislamu waliokuwa wakitekeleza ibada ya Swala ndani ya Msikiti wa al Aqsa kuondoka eneo hilo na kuwaruhusu walowezi wa Kizayuni kuvamia msikiti huo. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*