?>

Ongezeko la wanajeshi wa NATO nchini Iraq, juhudi za kujaza nafasi ya Marekani

Ongezeko la wanajeshi wa NATO nchini Iraq, juhudi za kujaza nafasi ya Marekani

Majeshi ya nchi za Magharibi yalipelekwa kwa wingi nchini Iraq baada ya Marekani kuivamia ardhi ya nchi hiyo mwaka 2003 na bado yanaendelea kuwepo nchini humo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Hata hivyo kwa kuzingatia sera za rais aliyeondoka madarakani wa Marekani, Donald Trump za kupunguza idadi ya wanajeshi wa nchi hiyo nchini Iraq hadi askari 2500, sasa Shirika la Kujihami la Nchi za Magharibi (NATO) linataka kuzidisha idadi ya askari wake nchini. 

Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg Alkhamisi iliyopita mwishoni mwa kikao cha Mawaziri wa Ulinzi wa nchi wanachama alitangaza kuwa, idadi ya askari wa shirika hilo nchini Iraq itazidishwa kutoka askari 500 hadi 4,000. Jens Stoltenberg amesema uamuzi huo umechukuliwa baada ya vikao vya Jumatano na Alkhamisi iliyopita vya shirika la NATO. Ameongeza kuwa, kwa sasa kuna wanajeshi wachache wa NATO nchini Iraq lakini idadi hiyo itazidishwa hatua kwa hatua. Katibu Mkuu wa NATO amedai kuwa, sababu ya kuchukuliwa uamuzi huo ni kuzuia uwezekano wa kundi la Daesh kupata nguvu tena nchini Iraq.

Uamuzi huo wa NATO unatambuliwa kuwa ni kubadilishwa siasa za hapo awali za shirika hilo kuhusiana na Iraq kwa asilimia 100. Kwani baada ya kushindwa kundi la Daesh nchini Iraq na kuongezeka mivutano ya kijeshi baina ya Iran na Marekani baada ya Washington kufanya mauaji ya kigaidi dhidi ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na vilevile maambukizi ya virusi vya corona, nchi wanachama wa NATO ziliondoa idadi kubwa ya wanajeshi wao nchini Iraq na kusitisha mafunzo kwa majeshi ya nchi hiyo. Sasa baada ya kushika madaraka rais mpya nchini Marekani na sera mpya za nchi hiyo kuhusu masuala mbalimbali, Mawaziri wa Ulinzi wa NATO wamechukua uamuzi wa kuzidisha mara 8 idadi ya wanajeshi wa nchi zao nchini Iraq kwa kisingizio cha kupambana na Daesh! Kwa sasa NATO ina wanajeshi 500 tu katika ardhi ya Iraq kwa ajili ya kile kinachodaiwa kuwa ni kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Iraq.  

Itakumbukwa kuwa mashambulizi ya Marekani ikisaidiwa na Uingereza dhidi ya Iraq hapo mwezi Machi mwaka 2003 ambayo yalipelekea kuondolewa madarakani utawala wa Baath na kukaliwa kwa mabavu nchi hiyo yalitambuliwa kuwa ni kinyume cha sheria baada ya kupingwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Hata hivyo tangu mwaka 2004 NATO, ikishirikiana na Marekani, ilichukua jukumu la kutoa mafunzo na ushauri kwa vikosi vya jeshi la Iraq. Tofauti na vikosi vya jeshi la Marekani na majeshi ya eti Muungano wa Kimataifa wa Kukabiliana na Daesh ambavyo vinafanya mashambulizi na hujuma katika maeneo mbalimbali ya Iraq, hadi sasa majeshi ya NATO yamejihusisha na kutoa mafunzo, ushauri na masuala ya kiufundi kwa jeshi na polisi ya Iraq.

Hata hivyo kupunguzwa askari wa Marekani katika ardhi ya Iraq hadi wanajeshi 2500 na mashambulizi yanayoongezeka kila uchao dhidi ya misafara na kambi zao za kijeshi, likiwemo shambulizi la karibuni katika uwanja wa ndege wa Erbil ambalo linatambuliwa kuwa ni tukio linalotia shaka, yote haya yamechukuliwa kama kisingizio tosha cha kuzidishwa idadi ya askari wa NATO nchini Iraq. Hapana shaka kuwa ongezeko hilo kubwa la askari wa NATO nchini Iraq halitaishia katika majukumu ya kutoa mafunzo; kwa msingi huo tunaweza kusema kuwa, wanajeshi hao wa NATO watachukua nafasi ya askari wa Marekani.

Mchambuzi wa kisiasa wa Iraq bwana Abbas al Ardawi anasema: "Tangazo la NATO kuhusu uamuzi wake wa kuzidisha mara 8 idadi ya wanajeshi wake nchini Iraq ni uvamizi dhidi ya nchi inayojitawala. Askari wa NATO kwa hakika ni wale wale wanajeshi wa Marekani (ambayo pia ni mwanachama wa NATO). Kwa msingi huo ni wazi kuwa madai ya kuzidishwa idadi ya askari wa NATO nchini Iraq ni mchezo mpya wa Washington katika nchi hiyo. Washington imechukua uamuzi wa kuhepa azimio la Bunge la Iraq lililoiamuru serikali ya Baghdad kuwafukuza wanajeshi wote wa kigeni nchini humo."

Nukta nyingine ya kuashiria hapa ni kuwa, kutimia kwa uamuzi huo wa NATO kutakuwa na maana ya kupanuliwa eneo la kijiografia la operesheni za NATO nje ya mipaka ya Ulaya. Wakati huo huo na kwa kutilia maanani azimio la Bunge la Iraq lililopasishwa baada ya Marekani kufanya mauaji ya kigaidi dhidi ya Kamanda Qassem Soleimani katika ardhi ya Iraq mwaka jana wa 2020, hatua hiyo ya NATO ni kujaza nafasi wanajeshi wa Marekani, na hapana shaka kuwa inakiuka sheria.  

342/Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni