?>

Onyo la makundi ya mapambano ya Iraq kuhusu kuondoka askari wa Marekani

Onyo la makundi ya mapambano ya Iraq kuhusu kuondoka askari wa Marekani

Kufuatia uvumi unaoenezwa kuhusu kutotekelezwa ratiba ya kuondoka askari wa Marekani katika ardhi ya Iraq, makundi ya mapambano ya nchi hiyo yametoa onyo kali kuhusu jambo hilo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Wanajeshi wa Marekani waliivamia Iraq mwaka 2003 kwa ajili ya kuung'oa madarakani mfumo wa kibaathi wa nchi hiyo uliokuwa ukiongozwa na Saddam Hussein. Wengi wa askari hao waliondoka nchini humo mwaka 2011 baada ya kutimiza wajibu wao. Pamoja na hayo, wanajeshi hao walirejea Iraq mwaka 2014 kwa ombi la serikali ya nchi hiyo kwa lengo la kuisaidia kukabiliana na magaidi wa Daesh ambao katika kipindi hicho walikuwa wameteka na kukalia thuluthi moja ya ardhi ya Iraq. Kwa kisingizio hicho Marekani ilituma Iraq maelfu na malefu ya wanajeshi chini ya mwavuli wa muungano wa kimataifa kwa ajili ya kupambana na Daesh ambapo sehemu kubwa ya askari wa muungano huo walikuwa Wamarekani.

Baada ya kushindwa Daesh mwaka 2017, kuendelea kusalia Iraq askari wa Marekani uligeuka kuwa mjadala mkubwa kwa sababu hakukuwepo tena na sababu ya kuhalalisha kuendelea kusalia nchini humo askari hao vamizi. Hatua ya Marekani ya kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) na Abu Mahdi al-Muhandis, Naibu Mkuu wa Jeshi la Kujitolea la Wananchi wa Iraq la Hashdu-Sha'abi karibu na uwanja wa ndege wa Baghad, iliamsha hasira ya watu na makundi ya kisiasa ya Iraq, na hasa yale yanayofungamana na mrengo wa mapambano.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*