?>

Pande zote zathibitisha kupigwa hatua katika mazungumzo ya nyuklia ya Vienna

Pande zote zathibitisha kupigwa hatua katika mazungumzo ya nyuklia ya Vienna

Mwakilishi wa Russia katika mashirika ya kimataifa yenye makao yao mjini Vienna amesema, pande zote washiriki katika mazungumzo ya nyuklia ya Vienna wamethibitisha kuwa hatua zimepigwa kwa ajili ya kufikia mwafaka juu ya mazungumzo hayo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mikhail Ulyanov amesema katika ujumbe alioandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa, hatua zimepigwa katika mazungumzo ya Vienna ya kuiondolea vikwazo Iran.

Ulyanov amebainisha: "hivi sasa washiriki wote katika mazungumzo ya Vienna wamethibitisha kuwa zimepigwa hatua kadhaa kuelekea mwafaka wa kuyafufua makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kuondolewa vikwazo, japokuwa kuna udharura wa kuendelezwa jitihada za ziada kwa ajili ya kufikia lengo hilo."

Duru ya nane ya mazungumzo ya Vienna, ambayo ajenda yake kuu ni kuondolewa vikwazo vya kidhalimu na visivyo vya kisheria ilivyowekewa Iran, ilianza Jumatatu iliyopita kwa kikao cha kamati ya pamoja ya JCPOA kilichofanyika chini ya uenyekiti wa Ali Baqeri, kiongozi wa ujumbe wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mazungumzo hayo na Enrique Mora, Naibu Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambayo ni nchi inayowajibika, imetangaza mara kadhaa kwamba, kwa kuwa Marekani ndiyo iliyokiuka makubaliano ya JCPOA, inapaswa iondoe vikwazo ili iweze kurudi kwenye makubaliano hayo na kuna ulazima pia utekelezaji wa makubaliano hayo utakaofanywa na Marekani uweze kuthibitishwa.../


342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*