?>

Papa Francis atoa maagizo ya kupambana na ufisadi baina ya viongozi wa Vatican, maaskofu na makadinali

Papa Francis atoa maagizo ya kupambana na ufisadi baina ya viongozi wa Vatican, maaskofu na makadinali

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani ameamuru kuwepo uwazi kamili wa kiuchumi na kifedha baina ya viongozi na wakurugenzi wa Vatican wakiwemo makadinali na kusimamiwa vyema utendaji wao.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Papa Francis pia amepiga marufuku viongozi hao kupokea zawadi zenye thamani ya zaidi ya Euro 40. 

Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa mwezi Mei mwaka jana pia Papa Francis alitoa amri ya kuwekwa sheria kali zinazohusiana na mikataba ya Vatican. 

Suala la kupeana zawadi baina ya viongozi wa kidini wa Kanisa Katoliki limeibua kashfa nyingi ndani ya kanisa hilo katika miaka ya karibuni. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*