?>

Papa Francis atoa wito wa kuchukuliwa hatua za kukomeshwa kuwatumikisha watoto

Papa Francis atoa wito wa kuchukuliwa hatua za kukomeshwa kuwatumikisha watoto

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani amewtoa wito wa kukomeshwa mtindo na tabia ya kuwatumikisha watoto katika maeneo mbalimbali ulimwenguni.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Papa Francis amesema kuwa, kuna haja ya kuchukuliwa hatua za kukabiliwa na mwenendo huu wa kutumikishwa watoto ambao kimsingi wanapaswa kuwa shuleni.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani amesema, huu ni katili kabisa ambapo watoto badala ya kujishughulisha na michezo wanalazimishwa kufanya kazi kama watu wazima au kuwaona katika majaa ya taka wakitafuta kitu kwa ajili ya kwenda kuuza.

Papa Fancis amesema: Njooni tuwafikirie wahanga hawa na kutafuta njia za kuweza kuhitimisha mwenendo huu wa kutisha wa watoto kufanyishwa kazi.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na Shirika la Kazi Duniani (ILO) na Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF), idadi ya watoto wanaofanyishwa kazi kwa lazima kote duniani imeongezeka na kupindukia milioni 160; hili likiwa ni ongezeko la juu zaidi kuwahi kuripotiwa tokea mwaka 2000.

Ripoti ya taasisi hizo mbili za Umoja wa mataifa imeonesha kuwa, watoto milioni 8.4 wametumikishwa kwa lazima katika kipindi cha miaka minne iliyopita, huku wengine milioni 9 wakiwa katika hatari ya kutumbukia kwenye kazi hizo za sulubu na kulazimishwa kufikia mwaka 2022 kutokana na janga la Corona.

Kwa mujibu wa UNICEF, bara la Afrika linaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watoto wanaofanyishwa kazi huku asilimia 43 kati yao wakiwa wanafanyishwa kazi za hatari.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*