?>

Papa Francis atoa wito wa kufanyika mazungumzo ya kusitisha ghasia Kazakhstan

Papa Francis atoa wito wa kufanyika mazungumzo ya kusitisha ghasia Kazakhstan

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani ametoa wito wa kufanyika mazungumzo kwa ajili ya kuhitisha ghasia na mgogoro ulioibuka nchini Kazakhstan.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Papa Francis ameonyesha kusikitishwa kwake na mauaji yaliyosababishwa na ghasia nchini Kazakhstan na kueleza kuwa, ana matumaini mgogoro huo utapatiwa ufumbuzi kupitia mazungumzo.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Kazakhstan imetangaza kuwa, zaidi ya watu 160 wakiwemo maafisa usalama wameuawa hadi sasa  tangu kuanza kwa machafuko katika nchi hiyo ya Asia ya Kati wiki moja iliyopita.

Watu hao wameuawa katika makabiliano ya siku kadhaa baina ya waandamanaji na maafisa usalama. Wananchi wa Kazakhstan walianzisha maandamano ya ghasia ya kulalamikia hatua ya serikali ya kupandisha bei ya mafuta.

Siku ya Jumapili, kulishuhudiwa utulivu kiasi katika mji huo ambao ndiyo kitovu cha uchumi wa Kazakhstan, ambapo polisi ilikuwa ikifyatua risasi hewani kuzuia watu kusogelea bustani kuu ya mji.

Msemaji wa Polisi ya nchi hiyo, Saltanat Azirbek amesema kuwa, makumi ya wafanya fujo wameuawa na maafisa usalama katika maandamano hayo katika mji mkuu wa kiuchumi wa Almaty, walipojaribu kushambulia majengo yenye ofisi za serikali.

Mkuu wa Polisi katika jiji la Almaty, Kanat Taimerdenov, amesema wanaofanya fujo na kuharibu mali za umma, mbali na kushambulia wananchi wenzao kwenye maandamano hayo ni watu wenye misimamo ya kuchupa mipaka.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*